30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

DK. BASHIRU: SITAONEKANA MAJUKWAANI

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally amesema hataonekana katika majukwaa ya siasa kwa sababu yeye ameteuliwa kuwa mtendaji  na si mwanasiasa wa chama hicho hivyo atatekeleza yale tu yanayoamriwa katika vikao vya Halmashauri Kuu.

Dk. Bashiru amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa ofisi na kutambulishwa kwa watendaji wa chama hicho, na Katibu Mkuu mstaafu, Abdulrhaman Kinana katika Ofisi kuu za chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.

“Mimi nimeteuliwa kuwa mtendaji wa chama kazi niliyopewa si ya jukwaaani, ni marufuku kwa watendaji kujihusisha na siasa hivyo watu wasitarajie kuniona katika majukwaa.

“Jukumu langu kubwa ni kutekeleza maazimio ya vikao, kutoa taarifa pamoja na kusimamia maagizo ya chama haya ni masuala ya mezani si ya jukwaani wapo waliopewa dhamana ya kukaa katika majukwaa,” amesema Dk. Bashiru.

Aidha, amesema atalipa kipaumbele suala la serikali kuhamia Dodoma ambapo katika miaka iliyopita walishindwa, hivyo ataanzia hapo na kuhakikisha wanafanikiwa na ataendelea pale walipoanzia.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles