24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Bashiru asema Lissu anaumwa deko

*Asema umanamba hauna nafasi Tanzania

MWANDISHI WETU-KILOSA

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), anaumwa ugonjwa wa deko huku akimuomba Rais Dk. John Magufuli aanze kutibu ugonjwa huo.

Kauli hiyo aliitoa juzi wilayani Kilosa mkoani Morogoro, katika ziara yake ya kikazi ikiwa ni sehemu ya maadhimino ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM, ambapo Lissu amekuwa akisema uongo katika nchi za Ulaya huku akiota siku moja atakuwa Rais wa Tanzania.

Wakati mtendaji huo wa juu wa CCM akiyasema hayo, Lissu amekuwa akiendeleas na ziara yake katika nchi za Ulaya ambapo kwa sasa yupo nchini Marekani akieleza kile alichodai hali ya demokrasia nchini na kupigwa kwake risasi.

Kutokana na hali hiyo Dk. Bashiru, alisema kuwa dalili za ugonjwa wa aina ya Tundu Lissu ni kusema uongo, dharau, deko, uonevu, kiburi, majivuno.

“Ila shukrani ya Punda ni mateke. Namuomba Rais wetu (Dk. John Magufuli) aanze kutibu ugonjwa wa deko unasomesha watu wanazunguka kutukana nchi yao na Rais wao kisa ugonjwa wa deko.

“Yupo msomi mmoja anaitwa Tundu Lissu ameugua ugonjwa wa deko, anadeka hajui jembe kwa maisha yake, hajui mpunga unalimwaje wala samaki wanavuliwaje.

“Hajapanda bodaboda muda mrefu na watoto wake hawasomi shule hizi anazunguka dunia nzima kutuchafua. Tunao Tundu Lissu wengi Serikalini tumewaamini tumewapa dhamana ila ukiwatembelea ofisini wanadeka, mara nyingine hawapo, wanajipendelea wao,” alisema Dk. Bashiru

Alitaja dalili za ugonjwa huo aliuta aina ya Tundu Lissu ni kusema uongo, dharau, deko, uonevu, kiburi, majivuno.

“Ugonjwa huu unaambukizwa na tumeulea na manesi na madaktari wa ugonjwa huu ni Watanzania nyie wenyewe. Huu Uugonjwa hatari, unaambukizwa ni hatari kuliko Ukimwi. Anasema tumeweka Kifungu kwenye Katiba ya CCM cha kuzuia watu kugombea urais sio kweli ni uongo,” alisema

Alisema dalili za ugonjwa huo wa deko ni ubinafsi, kuota urais wa Tanzania kuwa na kiburi na kwenda Ulaya kuzungumza lugha za wakoloni lakini sasa anayemwita dikteta amefuta mashamba kwa ajili ya wanyonge.

“Nilipomskiliza nikasema ni muongo na kwa sababu anaumwa ugonjwa unaitwa Tundu Lissu, basi yupo kwenye hali mbaya.

“Ugonjwa wa Tundu Lissu ni hatari ila unaponyeka amuache Rais (Dk. John Magufuli) atumikie wanyonge, watendaji wote wa serikali ambao hawataki kupona ugonjwa huu watafute serikali nyingine, ajira ni hiyari waandike barua waseme chama hiki hakipendi dhuruma, mimi nadhurumu, hakipendi uongo mimi Mmuongo uachie madaraka,” alisema

ARDHI NA UMANAMBA

Akizungumza migogoro ya ardhi, Dk. Bashiru Ally, alisema kuwa katu CCM haitokubali kuona Watanzania wanageuzwa manamba katika ardhi yao.

Alisema licha ya mashamba 40 kufutiwa umiliki badala ya kugeuka neema sasa imekuwa balaa huku akizitaka mamlaka ya serikali kujitathini na kutafuta ufumbuzi wa haraka katika suala hilo.

Hayo aliyasema juzi wilayani Kilosa mkoani Morogoro, katika ziara yake ya kikazi ikiwa ni maadhimino ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM, ambapo alisema kuwa usimamizi mbovu wa ardhi ni usaliti kwa wapigania uhuru wan chi.

“Nimekuja hapa Kilosa, hapa nimeitwa na wananchi ambao hawaridhishwi na namna ambavyo suala ya ardhi linashughulikiwa na vyombo vyenye mamlaka na mahusiano ya wakulima na mamlaka.

“Nimeambiwa kwamba mashamba ambayo yamefutwa badala ya kuwa neema yamezusha balaa. Ardhi ndio kielelezo cha uhuru wetu na uhai wetu, usimamizi mbovu wa Ardhi ni usaliti kwa wapigania uhuru wa nchi yetu.

“CCM haitamvumilia mtu ambaye atawageuza manamba Watanzania wengine na yule anayemiliki ardhi na haiendelezi,” alisema Dk. Bashiru

Katibu Mkuu huyo wa CCM alisema hakuna kiongozi wala tajiri nchini ambaye halishwi na maskini.

“Ni marufuku kuvunja haki za wazalishaji wadogo hasa maskini, ni marufuku kubadilisha ardhi kuwa bidhaa,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles