32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Bashiru apiga marufuku vikao vya fitina CCM

CLARA MATIMO Na YOHANA PAUL- MWANZA

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amepiga marufuku vikao vya fitina ambavyo vinalenga kujadili ajenda kabla ya wakati.

Alitoa onyo hilo jijini hapa mwishoni mwa wiki katika mkutano wa kuimarisha demokrasia mashinani uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Dk. Bashiru ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Mwanza,  alisema vikao vinavyoruhusiwa ni vile vinavyojadili utekelezaji wa ilani ya CCM, kero za wananchi na wanachama, kutatua migogoro kwa mujibu wa taratibu na  kufanya uteuzi wa watu wenye sifa.

“Najua tunaelekea kwenye vikao vya uchaguzi ni marufuku kuendesha vikao vya fitina vile vilivyozoeleka watu wanapanga na kujadili ajenda kabla ya wakati na wanatoka wamedhamiria kuchinja mtu,  pia ikiwa ni kikao cha siri, siri hizo zisivuje, katika kipindi hiki ndani ya CCM ni marufuku kulea na kufuga makundi ya vyeo.

“Kuna eneo nimesikia mtu mmoja amechinjwa baada ya kushinda kura za maoni wakampeleka mtu wa pili kwa kisingizio kwamba alikuwa Chadema sasa nasema hivi wote waliorudi CCM kwa kufuata utaratibu wa kikatiba tangu saa hiyohiyo wana haki na wajibu sawa na wanachama wengine.

“Kama vitendo vya kuchinja mtu vinafanyika mikoa mingine Mkoa wa Mwanza ambako mlezi ni mimi upokee pesa kwa njia yoyote halafu umwambie nitakupigia debe kwenye vikao, upitishe mtu asiye na sifa kisa ulisoma naye au mnajuana kwa namna yoyote ile hapa hakuna tena nafasi hiyo na ukibainika utachukuliwa hatua za kinidhamu,” alisema.

Aidha Dk. Bashiru alisema wataendelea kuboresha elimu ya msingi na sekondari kwa kuwajengea wanafunzi  mbinu za  kujitegemea  ikiwemo kukuza uwezo wa kufikiri, kuchambua mambo mbalimbali , kujiamini, kubuni na kupenda taifa lao .

“Tunataka watoto wetu wawe wabunifu na waweza kujiamini wasisome tu kwa ajiri ya kujibu na kufaulu mitihani na kujaza lundo la vyeti la hasha! tunataka wawe kama  viongozi wetu waliotangulia akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye tumampa sifa nyingi kutokana na kupata elimu yenye utaifa ndani yake.

“Wako wasomi mnawajua wanamalundo na magunia ya vyeti wengine wanaitwa maprofesa, wengine wasomi mawakili na wachumi lakini hawajiamini na hawana utaifa, msomi aliyesoma na kusomeshwa katika nchi hii hawezi kunyanyua kinywa chake kumtusi rais, usomi wa aina hiyo ni laana,” alisema na kuonya Dk. Bashiru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles