27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Bashiru amkaribisha Zitto CCM

FRANCIS  GODWIN Na RAYMOND  MINJA-IRINGA



KATIBU Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, amemkaribisha Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ajiunge na chama hicho.

Amesema hiyo ni kwa sababu Zitto ni miongoni mwa  wanasiasa wanaojua kujenga hoja za uchumi.

Pamoja na kutoa mwaliko huo, Dk. Bashiru alishangazwa na ukimya wa Zitto kuhusu suala la korosho kama alivyokuwa akijenga hoja kuhusu suala la mgodi wa Buzwagi uliopo mkoani Shinyanga.

Kauli hiyo aliitoa Iringa jana alipozungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa.

Alisema Zitto ni kijana mwenye uwezo wa kupambanua mambo ya uchumi kwa sababu  hata wakati wa suala la Buzwagi alionyesha uwezo mkubwa wa kupambanua mambo.

“Hakuna  kijana mzuri  mwenye  uwezo  wa  kupambanua  mambo ya  uchumi  nchini kama Kiongozi wa Chama  cha  ACT- Wazalendo Zitto Kabwe.

“Wakati wa suala la  Buzwagi  yeye ndiye  aliweza  kuonyesha  uwezo mkubwa wa kupambanua mambo kwa vile  hata mikutano yake  ilikuwa na mwitikio mkubwa  kutokana na umaarufu  alioupata kwa  hoja zake nzito za kujenga hoja bungeni.

“Ila leo wakulima  wa korosho  nchini  walikuwa  wakiminywa Zitto yupo kimya…  nasema  Zitto ni  kijana mzuri ila chama alichopo si cha kijamaa kama  CCM ni vizuri aje CCM  kuungana na chama cha kijamaa kinachopinga unyonyaji,” alisema Dk. Bashiru.

Hata hivyo,  Katibu Mkuu huyo wa CCM alishangazwa na ukimya wa viongozi wa vyama vya siasa wakati wa suala la korosho mikoa ya kusini.

“Uchunguzi  umeonyesha  wakulima  walikuwa wakinyonywa na  viongozi wa vyama vya siasa  wakiwamo  baadhi kutoka ndani ya CCM kama wabunge, mawaziri  na  ndiyo  sababu wengi  walichukizwa na serikali ya Rais Dk. Magufuli, kuchukua uamuzi wa kununua korosho hizo ila  sisi kama chama tunapongeza hatua hii amhayo sasa imekwenda kinyume na matakwa ya wanyonyaji wachache,” alisema

WALIOFUKUZWA

Dk. Bashiru  alitoa wito kwa viongozi na wanachama  wa CCM ambao walikuwa wanatumikia adhabu ikiwamo kufukuzwa unachama na kuvuliwa nafasi za uongozi kutokana na kujenga makundi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kuandika baru za kuomba msamaha na watasamehewa.

“Nataka  kutumia hadhara  hii kuwataka wale ambao  walisimamishwa, kuvulia uongozi na hata uanachama ndani ya chama chetu kuandika barua za kuomba msamaha  tutawasamehe maana chama hiki ni chetu sote.

“Tunatambua kutokana na yule waliyemtegemea  kuondolewa kugombea nafasi ya urais mwaka  2015 wengi  walisaliti  chama chetu na vikao vya juu vilifanya uamuzi wake ila wanaweza kuandika barua kuomba kusamehewa  tutawasamehe,” alisema Dk. Bashiru.

Pamoja na hali hiyo aliwataka wanachama wa CCM  kuendelea kuheshimu maadili ya chama hicho na maagizo mbalimbali yaliyotolewa na chama.

Alisema  hakutakuwa na msalie Mtume mwana CCM ambaye ameanza mchakatoi wa kujinga kwa ajili ya udiwani, ubunge ama urais.

Vilevile alishangazwa na kuibuka vurugu za kusaka urais wa Zanzibar mwaka 2020  kwa baadhi ya wana CCM kuanza kujenga makundi jambo ambalo ni kinyume na kanuni na katiba ya chama hicho tawala.

Alisema CCM ni chama kinachoendeshwa kwa misingi na si chama ambacho kiongozi wake anatokana na kuomba  kuchaguliwa bali hupatikana kwa utaratubu na si kujipitisha ama kugawa pikipiki, baiskeli au zawadi mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles