22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Dk. Bashiru aanza ziara ya siku 10 Z’bar

IS-HAKA OMAR -ZANZIBAR

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally anatarajia kufanya ziara ya siku 10  kisiwani Zanzibar kuanzia leo.

Dk. Bashiru anafanya ziara hiyo kwa mara ya pili tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo. 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Catherine Peter Nao, alisema maandalizi yote yamekamilika.

Catherine alisema katika ziara yake hiyo pamoja na mambo mengine, Dk. Bashiru atazungumza na viongozi mbalimbali, jumuiya zake na kuzindua miradi.

Alisema ziara ya Dk. Bashiru itakuwa ni ya kikazi, atatembelea maeneo mbalimbali na kutoa maelekezo. 

“Natoa wito kwa viongozi, watendaji na wanachama kujiandaa vizuri maeneo yao ambayo katibu mkuu wetu atatembelea,” alisema Catherine.

Alisema Dk. Bashiru alitarajia kupokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar (AAKIA) jana na ziara yake itaanzia Mjini Unguja.

Catherine alisema baada ya kukamilisha ziara Unguja, Desemba 2 hadi 4 ataendelea kisiwani Pemba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles