23.8 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

DJOKOVIC ATWAA TAJI LA QATAR OPEN

DOHA, QATAR


 

Tennis - Qatar OpenNYOTA wa mchezo wa tenisi raia wa nchini Serbia, Novak Djokovic, ameanza mwaka vizuri kwa kutwaa taji la Qatar Open dhidi ya bingwa namba moja kwa ubora duniani, Andy Murry.

Fainali hiyo ilikuwa ya kwanza kwa nyota hao kukutana kwa mwaka 2017, lakini Djokovic ambaye anashika nafasi ya pili kwa ubora duniani kwa upande wa wanaume, ameweza kumtembezea kichapo bingwa namba moja Murray.

Djokovic alionesha uwezo wake huku akishinda kwa seti 6-3, 5-7, 6-4 na alionekana kutumia nguvu nyingi sana katika mchezo huo ambao walitumia saa mbili na dakika 54.

Wataalamu wanadai kuwa katika mchezo huo wa juzi, Djokovic alionesha kiwango cha hali ya juu dhidi ya mpinzani wake tofauti walivyokutana katika michuano ya Barclays ATP World Tour, jijini London kwenye uwanja wa 02 Arena.

“Huu ulikuwa ni mchezo mgumu kwangu na ndio maana nimeupoteza, lakini naweza kusema kwamba ni jambo la kujivunia kuuanza mwaka, nimekutana na mpinzani ambaye ana uwezo mkubwa hivyo nimejivunza mengi kutoka kwake,” alisema Murray.

Kwa upande wa Djokovic, alisema haikuwa rahisi kupambana na bingwa namba moja, lakini anashukuru ameweza kuonesha moto wake na kuuanza mwaka vizuri.

“Nilikuwa na wakati mgumu kucheza na mpinzani mwenye uwezo mkubwa, nilifanya vizuri seti ya kwanza na yeye alifanya hivyo kwa seti ya pili, nakumbuka miezi mitatu ya mwisho mwaka jana sikucheza kama nilivyocheza sasa, hivyo kushinda dhidi ya bingwa ni kama ndoto,” alisema Djokovic.

Hata hivyo, Djokovic aliongeza kwa kusema kwamba, ameanza mwaka vizuri hivyo anaamini ataendelea kufanya hivyo hadi mwisho wa mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,719FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles