NYOTA namba moja kwa ubora duniani katika mchezo wa tenisi, Novak Djockovic, amefanikiwa kuchukua ubingwa wa wazi nchini Marekani baada ya kumchapa mpinzani wake, Rodger Federer, anayeshika nafasi ya pili kwa ubora duniani.
Novak amemshinda Federer kwa jumla ya seti 6-4 5-7 6-4 6-4, kutokana na ushindi huu mchezaji huyo jumla atakuwa ametwaa mataji matatu ya Grand Slam mwaka huu.
Mbali na kuchukua mataji matatu mwaka huu, mchezaji huyo hilo litakuwa ni taji lake la 10 la Grand slam tangu aanze kucheza mchezo huo.
Kwa upande wa wachezaji wawili wawili, Martina Hingis na Sania Mirza, wametwaa ubingwa wa michuano hiyo baada ya kuwashinda wapinzani wao, Yaroslava Shvedova na Casey Dellacqua kwa seti 6-3, 6-3.
Ushindi huu ni wa nne kwa mwaka huu kwa wachezaji hawa, huku ukiwa ni ushindi wao wa pili wa Grand Slam.