25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

DJ Khaled aongeza mtoto wa pili

New York, Marekani

RAPA na mwandaaji wa muziki nchini Marekani, Khaled Mohamed maarufu kwa jina la DJ Khaled na mke wake Nicole Tuck, wamefanikiwa kupata mtoto wa pili wa kiume.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, DJ Khaled aliposti picha mbalimbali akiwa akiwa kwenye chumba cha uzazi mara baada ya mke wake huyo kujifungua.

“Asante Mungu, asante malkia wangu Nicole, Dr Jin ubarikiwe sana, mwingine wa kiume amepatikana,” aliandika msanii huyo.

Msanii huyo hadi sasa hajaliweka wazi jina la mtoto huyo kama ilivyo kwa mtoto wake wa kwanza Asahd ambapo aliliweka wazi jina pamoja na picha mara moja baada ya kujifungua.

DJ Khaled alitangaza kuwa mke wake ni mjamzito Septemba mwaka jana, huku akisema wanatarajia kuongeza mtoto wa kurithi vitu vyao.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,526FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles