27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Diwani mbaroni kwa kuhamasisha kupigwa DC

Walter Mguluchuma -Katavi

JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi, limemkamata na linamshikilia Diwani wa Kata ya Ikuba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi, Emanuel  Washeri (43) kwa tuhuma za kuwahamasisha wananchi kulishambulia kwa kulipiga   mawe gari la Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rachel Kasanda ambae alikuwa kwenye gari hilo akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama waliokuwa wakifuatilia utaratibu wa mpango  wa stakabadhi gharani .

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana katika  Kijiji cha Kashishi Kata ya Ikuba  Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele

Alisema  siku hiyo  Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rachel  Kasanda alikuwa ameongozana na kamati yake ya ulinzi na usalama huku wakiwa na askari polisi wawili walifika kwenye Kijiji cha Kashishi Kata ya Ikuba kwa lengo  la ufatiliaji  wa mpango  wa stakabadhi gharani .

“Wakati wakiwa kwenye kijiji hicho walikamata gari  lenye  namba za usajili  T 924 DNE  aina ya Fuso mali ya  Matamba Enterprises iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Yusuph Zephania mkazi wa Sumbawanga  mkaoni Rukwa wakiwa wanapakia mazao aina ya ufuta nyumbani kwa diwani Emanuel  Washeri kinyuma na maelekezo ya kamati hiyo ya ulinzi na usalama.

Kamanda  Kuzaga alisema ndipo lilipotokea kundi la vijana  lililokuwa likiongozwa  na watu wawili ambao ni Mwandu  Ngarika(25) na  Bila  Charles(28) walihamasishwa na diwani huyo kufanya fujo kwa mkuu huyo wa Wilaya ya Mlele .

“Baada ya kuhamasishwa  walianza kufanya fujo  kwa kumrushia mawe Mkuu wa Wilaya Rachel Kasanda pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama  .

“Hali hiyo  ya vurugu ilipelekea  askari  polisi waliokuwa kwenye msafara huo kuchukua hatua  ya kuwatawanya watu hao ili kumwokoa  Mkuu huyo wa wilaya asiodhurike na  watu hao,” alisema 

Kamanda Kuzaga alisema askari hao walifyatua  risasi  za moto hewani  na mabomu  matatu  ya kishindo  ambayo hata hivyo hatakuleta madhara kwa wananchi .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles