23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Diwani mahakamani kwa kumpa mimba mwanafunzi

Upendo Mosha-Hai

DIWANI wa Kata ya Masama Mashariki, Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, John Munisi (38), amefikishwa mahakamani akidaiwa kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi.

Munisi alifikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo jana na kusomewa mashtaka mawili ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Marire mwenye miaka 17.

Akimsomea mashtaka mbele ya Hakimu Devotha Msofe, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Lubulu Mbise, alidai kuwa mshtakiwa ambaye ni diwani kupitia Chadema, alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti.

Mbise alidai kuwa alitenda kosa la kwanza katika Kijiji cha Ngira wilayani humo ambako alimbaka mwanafunzi  huyo Aprili 4, kosa alilotenda akijua ni kinyume cha sheria. 

 Alidai kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa  la ubakaji kinyume na  kifungu 130(1)(2)  na kifungu 131 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura 16  ya sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2000.

Mbise alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa la pili  katika kijiji hicho  hicho kwa kumpa ujauzito mwanafunzi huyo Aprili  kinyume na sheria ya elimu kifungu 60(A)(2) na (3)  iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mara baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa alikana kuyatenda  na Hakimu Msofe aliahirisha shauri hilo hadi Julai 29.

Mshtakiwa huyo yupo nje kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ambayo yalikuwa ni kuwa na watu wawili kila mmoja kuwa na barua inayotambuliwa kutoka kwa Serikali za mtaa au mtendaji na bondi ya Sh milioni mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles