22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Diwani Kimwanga aeleza miradi ya maaendeleo aliyotekeleza Makurumla

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Diwani wa Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo Mkoani Dar es Salaam, Bakari Kimwanga, ameeleza miradi mbalimbali ya maendeleo aliyotekeleza ndani ya miezi sita tangu alipochaguliwa katika kata yake.

Hayo ameyasema kwenye mkutano wa hadhara wa diwani huyo uliofanyija katika Mtaa wa Kilimahewa, ambapo amesema ndani ya miezi sita amefanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo ya ujenzi wa Barabara wenye dhamani ya bilioni 19.7 za kiwango cha lami na changarawe.

Amezitaja barabara hizo ni Barabara ya lami inayogenjwa kupitia DMDP inayotoka NIT, Mburati na Makurumla ambayo sasa ipo kwenye hatua ya kukamalizika kwamradi huo.

“Mlipotuchagua Mheshimiwa Mbunge wetu Profesa Kitila Mkumbo, alishirikiana nasi ikiwamo kufanya vikao na DMDP ambapo tulisukuma kutelezwa kwa mradi huu wa barabara hii ya lami. Tulifanya vikao na wananchi nikawaeleza umuhimu wa barabara nao wakapisha kwa kubomoa wenyewe nyumba zilizoingia kwenye hifadhi, asanteni sana.

“Lakini pia sikuchoka nikapambana ikiwamo kuwaleta Tarura hapa Barabara ya Mloka pamoja na Mbunge na kuwaeleza umuhimu wa barabara hii ambayo ilikuwa na handaki kubwa na siku moja mama mjamzito alijifungua kwenye shimo.

“Mbunge akanielewa akawataka Tarura kufanya tathmini ya kina na kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo akatupa Shilingi milioni saba, tumejenga na sasa gari zinapita na mreji upo sasa nawaomba tuitunze,” amesema Kimwanga

Aidha amewataka wananchi kuacha kusikiliza maneno ya wapotoshaji huku akiweka wazi kwamba bado joto la siasa za Uchaguzi Mkuu halijaisha kwani baadhi aliombanao nao kwenye kura za maoni wamekuwa mabingwa wakufyatua kila uongo ili kutafuta kivuli cha kujificha.

“Wapuuzeni hao, mimi tangu nimeapishwa hadi sasa nina miezi saba wapo watu wanapita wamegeuka walisha maneno watu kinywani mwangu, wapuuzeni sasa ni wakati wa kazi nataka mnipime baada ya miaka mitano muone nimefanya nini, lakini hata kwa miezi sita hii nimejenga barabara, miundombinu ya elimu Shule ya Mianzini yenye thamani ya Sh Milioni 50 ambayo ni fedha inayotokana na mapato ya ndani ya halmashauri.

Katika mkutano huo ambao ulidhuriwa na watalaamu kutoka Tanesco, Dawasa, Tarura pamoja na Jeshi la Polisi walipata fursa ya kuzungumza na wananchi ambapo walieleza kwa kina miradi inayotokelezwa kwenye kata ya Makurumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles