24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Diwani CUF auawa kwa kukatwa mapanga

Na Renatha Kapaka, Bukoba

DIWANI wa Kata ya Kimwani Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Silvester Miga (55) wa Chama cha Wananchi (CUF), amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitalini, baada ya kuvamiwa na kukatwakatwa  mapanga nyumbani kwake.

Tukio la kuuawa kwa diwani huyo lilitokea usiku wa kuamkia jana, akiwa nyumbani kwake akiangalia taarifa ya habari katika runinga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi, alisema Miga alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kagondo wilayani Muleba.

Ollomi  alisema tukio hilo lilitokea   wakati diwani huyo akiangalia runinga nyumbani kwake.

“Wahalifu  walivamia na kufanya mauaji haya kwa kumshambuliwa Miga kwa mapanga  na   kutoweka kusikojulikana.

“Baada ya hali hiyo alichukuliwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Kagondo kwa matibabu lakini kutokana na kujeruhiwa vibaya na kutokwa na damu nyingi alifariki dunia majira ya saa  saba usiku,” alisema Kamanda Ullomi.

Alisema   Jeshi la Polisi lilifanya msako na kuwatia mbaroni watu wawili ambao wanadaiwa kuhusika na tukio hilo.

Kamanda aliwataja waliokamatwa kuwa ni Aderarid Antony (42) na Shiranga Gonzari (22) ambao  jeshi hilo linaendelea kuwahoji.

Hata hivyo   baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Muleba wamesema  kuuawa kwa diwani huyo kuna mazingira ya  siasa.

Wananchi hao walilitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi   ili waliofanya mauaji hayo wabainike na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,093FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles