28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Diwani Chadema ajiuzulu na kuhamia CCM

Upendo Mosha-Moshi

ALIYEKUWA Diwani wa kata ya Kibosho Magharibi katika halmashauri ya wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema) Deo Mushi, amejiudhulu nafasi hiyo na kujiunga na chama Cha mapinduzi CCM.

Diwani huyo ambaye pia alikuwa Katibu mwenezi wa  Chadema wilaya ya Moshi, ametangaza kujiudhulu nafasi hiyo leo Jumamosi Aprili 27 wakati wa kukabidhiwa kadi ya CCM na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi.

Akizungumza,mara baada ya kutangaza kujiudhulu amesema, ameamua kuchukua uamuzio kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Maendeleo zinazolewa na serikali chini ya Rais John Pombe Magufuli.

“Nimeamua kujivua uanachama wa Chadema na vyeo vyangu vyote kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya Tano ya kuwaletea watanzania Maendeleo tofauti na wenzangu kwani Sina Imani ya ya kupata maendeleo kwenye halmashauri hii iwapo  tukisimamiwa  na Baraza la madiwani na wabunge wa Chadema”amesema

Akizungumzia suala hilo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Kastory Msigala, amethibitisha kupokea barua ya kujihudhulu kutoka kwa Diwani huyo na kwamba hatua inayofuata ni kuandika barua kwa mamlaka husika kwamba kata hiyo ipo wazi ili uchaguzi ufanyike.

Awali akimkabidhi Kadi ya CCM Boisafi amesema CCM imempokea Diwani huyo kwa mikono miwili na kwamba chama hicho hakina mgogoro nao wale wote wenye lengo la kujiunga nao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,908FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles