27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Diwani CCM akataliwa na wananchi, wadai ni mchawi wa maendeleo

BENJAMIN MASESE – SENGEREMA

Diwani wa Kata ya Chifunfu Wilayani Sengerema Robert Madaha (CCM),  amekataliwa na wananchi zaidi ya 2000 huku wakimtaja  hadharani kwamba ni adui namba moja wa  kukwamisha shughuli za maendeleo yao hususan katika sekta ya elimu kitendo kinachosababisha wanafunzi kupata mimba na kukatisha masomo ya sekondari.

Uamuzi wa pamoja  wa wananchi hao wakiongozwa na wajumbe wa Serikali za kijiji  ulifikiwa juzi katika mkutano wa hadhara  uliofanyika katika eneo inapojenjwa shule mpya ya Sekondari ya Bugumbisiko ambapo walidai sababu kubwa ya kumkataa diwani huyo ni kitendo chake cha kutoshirikiana nao au kuchangia chochote tangu ujenzi huo uanze mwaka 2018.

Pia  wananchi hao ambao walikuwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, walidai kwamba diwani huyo amekuwa  akifanya fitina  ndani ya vikao vya halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ili shule hiyo isiezekwe akidai majengo hayo yatatumiwa na popo na si wanafunzi wa Kijiji cha Chifunfu.

Baadhi ya mabango yalisomeka , Mheshimiwa Rais Magufuli umbali wa shule ndio chanzo cha mimba Chifunfu, Waziri Seleman Jaffo tuunge mkono kwani diwani wetu hajachangia hata 100 na shule hataki, tunakuomba ututembelee kwetu Chifunfu’.

Akisoma taarifa za kamati ya ujenzi wa sekonadari ya Bugumbisiko, Katibu wa kamati hiyo Fredick Nyamwanda, alisema wananchi waliamua kuanzisha ujenzi wa shule hiyo baada ya shule ya kata iliyopo sasa kujengwa mbali na kijiji hicho ambapo watoto hutembea kilimito 19 ili kuifikia ambapo wengi hushindwa kumaliza masomo kutokana na mimba zinazotokana na vishawishi wanavyopata njiani.

Akijibu tuhuma hizo Madaha alisema si kweli na kwamba amekuwa akijitahidi kumshawishi Mkurugenzi wa Sengerema ili kuwaezekea madarasa hayo ili shule iweze kusajiliwa na kuanza masomo mwakani.

“Jamani binafsi nasikitika sana juu ya malalamiko yenu na uamuzi wenu wa kuniita mchawi wa maendeleo yenu, ninajua tatizo ni siasa  mnazichanganya na shughuli za maendeleo, kwanza mngejua ninavyopambana  juu ya shule hii msingekuwa mnanisema vibaya hivi naombeni muache masuala ya mitaani ili tujenge shule hii,” alisema.

“Kwanza niwahakikishie hadi sasa bajeti ya kuezeka madarasa haya imetengwa katika bajeti inayoanza Julai Mosi mwaka huu, hivyo niwaomba wote tuwe wavumilivu, masuala ya kusema majengo yatakuwa ya popohayo ni mabo ya kwenye baa, kwanza niwafikishie salamu zenu mnasifiwa sana kwa kujenga shule imara yenye ubora sana,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles