24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

DIT yatoa mafunzo ya Tehama kuimarisha vifaa

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

TAASISI ya Teknolojia ya Dar es Dar es Salaam (DIT) imeanza kuendesha mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kwa walimu wa shule za serikali nchini.

Mafunzo hayo ambayo yanajulikana kitaalamu ‘Basic ICT Devices Maintenance and Repair’ ya siku tano yameanza jana na yatamalizika Oktoba 25, mwaka huu yamelenga kuimarisha utunzaji wa vifaa vya Tehama ambavyo hutolewa kwa shule mbalimbali nchini na serikali na wadau wengine.

Mratibu wa mafunzo wa DIT, Daudi Mboma, amevitaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na kompyuta, printa na vifaa vya mawasiliano.

“Mafunzo hayo yanayotolewa na wataalamu wa DIT yamefadhiliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (UCSAF) na walimu wanaohudhuria mafunzo hayo ni wa Shule za Msingi na Sekondari.

“Serikali hutoa vifaa mashuleni kama kompyuta, printa au vifaa vya mawasiliano kupitia UCSAF, imeonekana kuwa ni muhimu vifaa hivyo vikatunzwa vizuri hivyo tutoe mafunzo kwa walimu hawa ili waweze kutunza na kufanya ukarabati,” alisema Mboma.

Alisema jumla ya walimu waliopokelewa ni 540 kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Pwani, Mtwara, Ruvuma, Lindi, Kilimanjaro, Kilimajaro, Arusha, Manyara, Dodoma, Zanzibar na Tanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles