27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

DIT kusaidia SKUA kuandaa mtaala

Mwandishi Wetu

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), imeahidi kuisaidia Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga Tanga (SKUA) kuandaa mtaala wa uhandisi umeme moja na masuala ya rada katika shule hiyo.

Kaimu Mkuu wa Chuo Taaluma na Mafunzo wa chuo hicho, Dk. Ezekiel Amri ametoa ahadi hiyo jana alipokuwa akizungumza na timu ya wakufunzi waliofika chuoni hapo jana ambapo alisema kuwa ujumbe huo umekuja sehemu sahihi kwani wao wamebobea katika katika sekta hiyo.

“Ninataka niwahakikishie kwamba mlipokuja kupata msaada ni sehemu sahihi kabisa na sisi tunaahidi kuwasaidia ili muweze kufanikiwa katika hilo. DIT kwa hapa nchini tumebobea hasa na mitaala yetu ni bora,” amesema Dk Ezekiel.

Naye Mkuu wa mradi wa Kituo Cha Umahiri wa Tehama cha Kikanda (RAFIC), Joseph Matiko amesema kuwa fedha za mradi huo zinaweza kukisaidia chuo hicho cha Kijeshi kupata mtaala wake.

“Kwa upande wa mradi Mimi nitawasikisha hilo ili muweze kupata msaada wa fedha pia mnaweza kusema wataalamu mnaowahitaji kutengeneza wataalamu wa kuandaa mtaala huo hii ni kuonesha kwamba sisi kama DIT tuko tayari kuwasaidia,” amesema Dk. Matiko.

DIT imejipambanua katika kutoa utaalamu ambao unatatua matatizo katika jamii na kutoa wataalamu wa hali ya juu katika kutimiza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles