30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 9, 2021

‘Dirisha Moja’ kupunguza msululu ulipaji kodi TRA, TPA

BethshebaWambura, Dar es Salaam

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kushirikianana Mamlaka ya Bandari (TPA), ziko katika hatua za mwisho za kutengeneza mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya mtandao (Dirisha Moja) ili kurahisisha ulipaji kodikwa wafanyabiashara.

Akizungumza leo Jumatatu Desemba 10, katikakikao cha Rais John Magufuli, uongozi wa TRA na wakuu wa mikoa nchini kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema hadi kufikia mwakani mfumo huo utakuwa tayari.

Amesema TRA na TPA wanatarajia mfumo huo kuwawezesha wafanyabishara kulipia katika mfumo mmoja kisha idara hizo zitagawana mapato nasi mfanyabiashara kulipia kila mmoja kivyake na hii itaipunguzia serikali gharama za uendeshaji.

“Tunajitahidi kila siku kuongeza uboreshaji wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato kama vile kodi ya majengo, kampuni za simu na mabenki.

“Na hii ndiyo sababu tunataka kuleta mifumo rafiki na rahisi ya ulipiaji kodi ambapo mfanyabiashara anaweza kulipa wakati wowote na sehemu yoyote,” amesema Kichere.

Amesema pamoja na kuwa wanajitahidi kukusanya kodi lakini wana changamoto hasa katika mfumo wa sasa wa ulipaji kodi kwa kutumia mashine za kieletroniki (EFD) una na shida kwani mtu hawezi kutambua ipi risiti ya kughushi na ipi halali hadi awe mtaalamu na hii inasababisha fedha nyingi kupotea hivi sasa wanafanya mpango ili watu wahakiki risiti hizo kwa kutumia simu zao.

“TRA imefanikiwa kuongeza ukusanyaji wa kodi kutoka sh bilioni 850 kwa miaka mitatu iliyopita hadi Sh trilioni 1.3 kwa mwezi na tutaendelea kukusanya zaidi ya hapa kwani miradi mingi mikubwa inatekelezwa kutokana na fedha za kodi,” amesema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,702FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles