25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Director P kutoka Canada afunguka kuhusu ‘Masoko na Dollar’

Toronto, Canada

MWISHONI mwa miaka ya 90 kwenye Mji wa Kitwe nchini Zambia katika familia ya Mzee Lualua Lupasa alizaliwa kijana Patrick a.k.a Director P ambaye kwa sasa ni msanii wa kizazi kipya anayeishi Toronto, Canada.

Director P amekuwa na mchango mkubwa kwa wasanii wenye asili ya Afrika Mashariki huko Toronto kwani mbali na yeye mwenyewe kuimba ni prodyuza na mwongozaji wa video katika studio zake za Lupasa Records akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji.

Anasema mnamo 2012 aliondoka Afrika na kuhamia Canada huku akifuata nyayo za babu take ambaye alikuwa mchekeshaji nchini Kongo pamoja na baba yake ambaye alikuwa ni DJ, mchekeshaji na MC.

“Nimekuwa nikitaka kuwa kwenye tasnia ya muziki lakini mwaka 2019 ndipo nilianza rasmi kisha kuanza kutoa muziki wangu mnamo 2020,” amesema Director P.

CHANGAMOTO

Akiwa kama msanii kutoka Zambia anayeishi Canada, Director P anasema :” Kwangu mimi kama msanii huru na mchanga ninayekuja kwa kasi hapa Toronto changamoto ambayo nakabiliana nazo in muda kwasababu bado nasoma pia bei ya kurekodi audio na video zenye ubora kwa huku ni gharama sana.”

KOLABO

Director P anasema mbali na wasanii wengi wa Afrika kutamani kufanya kazi na mastaa wakubwa kama Diamond Platnumz, Harmonize na wengineo yeye anatamani kufanya kolabo na wasanii wenye majina ya wastani kama vile Swat Matire, Maandy, Kelechi Africana na Noti Flow.

ANAIPENDA ZAIDI AFRIKA

Licha ya kuishi ughaibuni lakini msanii huyo aliyewahi kutamba na nyimbo kama Ninaamini Mama na Nionyeshe anaamini katika kulipenda zaidi soko la muziki wa Afrika.

“Nimeamua kujitangaza barani Afrika kwa sababu nina amini sisi kama waafrika tuna uwezo mkubwa katika uwanja huu wa muziki na kwangu Afrika itakuwa nyumbani kila wakati,” amesema Director P.

MIPANGO YAKE

Director P anasema anatarajia kutembelea Tanzania mwaka ujao na kufanya kazi na wasanii wakubwa ili kujiongezea mashabiki na hivi karibuni ataachia wimbo wake mpya utakaotikisa chati mbalimbali za muziki.

“Nina wimbo wangu nitautoa hivi karibuni unaitwa Masoko na Dollar naamini utafanya vizuri kwasababu ni ujio wangu mpya baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu,” amesema Director P.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles