23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

DIOUF AITABIRIA MAKUBWA SENEGAL

LIBREVILLE, GABON


MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Taifa ya Senegal, El Hadji Diouf, anaamini kuwa kikosi cha sasa cha timu hiyo kitakuja kufanya makubwa katika michuano mingine licha ya kutolewa kwenye robo fainali za Mataiafa Afrika nchini Gabon.

Senegal ambao walipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika michuano hiyo, juzi walishindwa kuonesha uwezo wao na kujikuta wakitolewa kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi Cameroon.

“Ninaamini kwa baadaye timu hii itakuja kuwa bora zaidi ya sasa, lakini wachezaji wanatakiwa kuonesha umoja wa hali ya juu kwa kuwa soka ni mchezo wa akili pamoja na nguvu.

“Tunatakiwa kuwaunga mkono kwa hali na mali hili kufikia malengo ya taifa, lakini tunatakiwa kuwapongeza wapinzani wetu Cameroon kwa kuwa wametuonesha kuwa soka ni mchezo ambao unataka umoja na si uwezo wa mchezaji mmoja mmoja.

“Hata hivyo, kwenye matuta timu yoyote inaweza kushinda na nyingine kufungwa, hatukuwa na sababu ya kupoteza lakini ndivyo soka lilivyo.

“Siku zote tumekuwa na wakati mgumu tukikutana na Cameroon, nakumbuka tulipoteza dhidi yao katika fainali ya mwaka 2002,” alisema Diouf.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles