26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Dini ina mchango mkubwa wa kujenga maadili kwenye Taifa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa viongozi wa dini waendelee kupiga vita vitendo vya mmomonyoko wa maadili kwa jamii ili kulifanya Taifa kuwa mahali salama kwa watoto na Watanzania kwa ujumla.

Ametoa wito huo leo Ijumaa (Aprili, 14, 2023) alipofungua msikiti wa ‘Masjid Ali Bin Saif’ uliopo Vingnguti jijini Dar es Salaam. Msikiti huo umejengwa na familia ya Sheikh Seif Ali Seif.

Amesema kuwa moja kati ya msisitizo mkubwa wa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni katika kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto, mmomonyoko wa maadili

“Tukiachia mmomonyoko wa maadili, tunaweza kutengeneza Taifa ambalo halitakuwa na manufaa mbeleni, Viongozi wa dini mmekuwa mstari wa mbele katika kukemea ukatili dhidi ya watoto,” amesema Mjaliwa.

Majaliwa amesema kuwa ni budi kwa Watanzania kuhakikisha wanapiga vita matendo yote yanayoharibu utamaduni, mila na desturi ya mtanzania.

“Tunayoyasikia huko duniani tuombe yasije hapa nchini na kama yapo tuyapige vita, Taifa hili leo tupo hapa na viongozi walioongoza nchi hii walisimamia kwenye mapambano dhidi ya mmomonyoko wa maadili,” amesema Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka waumini wa dini ya kiislam kuutumia mwezi mtukufu wa ramadhan kuliombea taifa ili mwenyezi Mungu aendelee kuilinda na kudumisha amani, kuikinga dhidi ya maradhi na majanga mengine.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema amesema amevutiwa na ubora na uzuri wa msikiti huo. “Msikiti wa Ali bin Saif umejengwa kwa viwango vya juu sana hadi natamani na mimi pia ningekuwa mkazi wa Vingunguti ili na mimi nipate raha ya kusali kwenye Msikiti huu,” amesema.

Naye Kaimu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Omar ameipongeza familia ya Sheikh Seif Ali Seif kwa kujenga msikiti huo kwani ni sehemu bora kuliko sehemu zote duniani

Akizungumzia kuhusu msikiti huo wenye hadhi kubwa ambao umejengwa kwa niaba ya Baba yao ambaye ameshatangulia mbele ya haki. Sheikh Seif Ali Seif amesema msikiti huo unauwezo wa kuhudumia wanaume 600 na wanawake 150, ina vyumba vya madrasa 3

Pia katika ufunguzi huo ilifanyika ibada maalumu ya Kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wote wanaomsaidia majukumu yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles