23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Diamond: Wasanii Wasanii tupunguze chuki

Anna Potinus

Msanii Nasseb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema ifike mahali wasanii waanze kushirikiana katika mambo mbalimbali ili kuondoa uchonganishi unaofanywa na baadhi ya watu wakiamini kuwa kuna ugomvi kati ya wasanii jamboa ambalo sio kweli.

Diamond ametoa kauli hiyoleo Jumatatu Novemba 11, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema wasanii wanapaswa kuachana na dhana ya kuchukiana bilasababu na badala yake washirikiane kwakuwa mashabiki ni wa wote.

“Zamani kulikuwa na mambo ya uchonganishi sana yani jambo la Z Anton siruhusiwi kufika, sisi kama wasanii tunataka tutengeneza hela ina maana kama wadau hawapo sisi wenyewe tuanze kuwa wadau tupeane riziki lakini ninashukuru Mungu kupitia Wasafi festival tumeifuta hiyo taswira na mimi mkiwa na jambo lenu nialikeni maana tukikaa mbali ndo tunachonganishwa tunachukiana bila sababu.

“Yani unakutana na mtu hampendi tu Madee sasa kakufanya nini, Tanzania ina mikoa zaidi ya 26 wewe unaweza ukafanya shoo Mwanza mimi nikafanya Arusha mwingine Bukoba kila mtu na sehemu yake sasa tuchukiane kwasababu gani, mashabiki wenyewe hao hao ukiwaambia kama unanipenda weka mikono juu na mimi nikisema wataweka shabiki wangu ni shabiki wa mtu mwingine.

“Tunachonganishwa kwa vitu vya uongo kila mtu ana mafanikio yake kwenye upande wake na sehemu yake kila mtu ni raisi kwenye kazi yake cha muhimu ni kwamba kama havunji sheria za nchi, wewe ndio baba wa familia nyumbani kwako ukifika wanakuheshimu kwahiyo kila mtu ana heshima yake tusidanganyane,” amesema Diamond.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,411FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles