Diamond Platnumz atoa neno kwa wasanii

0
1339

BRIGHITER MASAKI, DAR ES SALAAM

STAA wa muziki nchini, Naseeb Abdul, ‘Diamond Platnumz’ amewataka wasanii wenzake kutumia vivutio vya Taifa katika kazi zao ili kutangaza utalii uliopo nchini.

Diamond Platnumz amesema kwa upande wake yupo tayari kutangaza vivutio mbalimbali kwa ajili ya kuitangaza nchi yake kupitia kazi zake.

“Haiwezekani mastaa kutoka nchi zingine kutembelea vivutio vyetu wakati sisi wenyewe tupo karibu na tunashindwa kwenda, mastaa wengi wamekuja nchini kama vile David, Beckham, Lionel Messi wamepanda mlima wetu Kilimanjaro.

“Nimefurahi kupanda Kilimanjaro japokuwa sikufanikiwa kufika kileleni, lakini kwangu ni jambo la kubwa na historia, hivyo wasanii kupitia kazi zetu inabidi tutangaze vivutio vyetu ili watalii waje, nchi ijulikane na tukuze uchumi wetu,” alisema msanii huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here