29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

Diamond Platnumz alamba dili nono Warner Music Group

Na Christopher Msekena, Dar es Salaam

Lebo kubwa ya Muziki duniani, Warner Music Group imetangaza kuingia mkataba wa kushirikiana na nyota wa muziki nchini, Naseeb Abdul Juma a.k.a Diamond Platnumz na lebo yake ya WCB.

Warner yenye makao makuu yake New York nchini Marekani kwenye ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Instagram imetangaza mkataba huo mpya na Diamond kupitia tawi la Afrika Kusini.

Kampuni hiyo imesaini makubalino na Diamond yatakowapa uwanja mpana wa kusimamia kazi zake zote, mauzo, uendeshaji, kusimamia ziara zake na mengine mengi.

Ushirikiano mpya huu pia utasaidia usambazaji wa kazi zote za Diamond Platnumz na wasanii wote walio chini WCB Wasafi hivyo kufanya msanii huyo kuwa lebo moja na Burma Boy wa Nigeria.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles