Diamond awaza kupagawisha Qatar 2022

0
887

Na GLORY MLAY

BAADA ya kunogesha usiku wa sherehe za tuzo za mchezaji bora wa Afrika (CAF), huko Hurghurda nchini Misri, nyota wa muziki nchini Tanzania, Nasib Abdul ‘Diamond Platinum’ amesema anatamani kupata nafasi kama hiyo kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Diamond alisema si kazi nyepesi kuitwa lakini anaamini hatua aliyofikia upo iwezekano mkubwa wa kupata nafasi kama hiyo.

“Tumuombe Mwenyezi Mungu kwani matarajio na ndoto zangu ni hizo, niwashukuru mashabiki na watu wangu wakaribu ambao wamenisapoti hadi kufika nilipofika na wazidi kuniombea nifike Qatar 2022,” alisema.

Msanii huyo amekuwa na jina kubwa barani Afrika na Ulaya kutokana na kufanya matamasha mbalimbali duniani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here