24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Diamond ampoteza Davido

 JESSCA NANGAWE 

KIONGOZI wa lebo ya WCB, Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platnumz ameweka historia nyingine baada ya kutajwa kuwa msanii namba mbili kwa mafanikio Afrika kupitia mtandao wa Youtube. 

Kwa mujibu wa Jarida la Billboard nchini Marekani, msanii huyo amekuwa mmoja kati ya wasanii wanaotumia vizuri mtandao wa Youtube kufanya mambo makubwa. 

Msanii namba moja anayefanya vizuri kwenye mtandao huo ni Burna Boy kutoka Nigeria huku Diamond Platnumz akishika nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikishikwa na Davido. 

Meneja wa Youtube, Kevin Meenan ameeleza kushangazwa na mafanikio ya Diamonda ambaye ana wafuasi milioni 3.6 ambao ni sawa na asilimia 80 ya wanaotazama video zake wanatokea nje ya Tanzania. 

Baada ya kupata taarifa hiyo Diamond alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii na kusema ‘Kufanya kazi kwa bidii, kusali na kujiamini ndio siri iliyojificha nyuma yake.’ 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles