31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Diamond amchangia Makonda madawati 600

DIAMOND-PLATNUMZNA THERESIA GASPER

KAMPUNI ya Wasafi Classic ‘WCB’ imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, madawati 600 kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa shule za msingi za jijini Dar es Salaam.

Serikali ilikuwa ikihitaji madawati 10,000 kwa ajili ya kusaidia wanafunzi ili kusiwe na watakaokaa chini.

Mkurugenzi Mtendaji wa WCB, Abdul Nassib ‘Diamond’, alisema aliahidi kitu kidogo atakachokuwa anapata atasaidia jamii na ameanza kwa shule za Dar es Salaam na baadaye ataelekea mikoani.

Hata hivyo, ameomba kati ya madawati hayo waliyoyatoa Shule ya Msingi Tandale ambayo amesoma isisahaulike katika msaada huo.

Naye Makonda alisema Diamond amekuwa mmoja wa wasanii wa kwanza kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli.

“Kuna watu wenye uwezo lakini hawajafanya kitu kama alichofanya Diamond japo tunafahamu kutoa ni moyo, hivyo nawaomba kundi hili wasiishie hapa liweze kujiwekeza katika uchumi au kilimo ili kufika mbali zaidi,” alisema.

Wakati huo huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa WCB, Said Fella, alimuomba Makonda adhibiti kazi za wasanii ili zisihujumiwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles