25.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 4, 2022

Diamond aipa nguvu ‘Wasted Energy’ ya Alicia Keys

 WIMBO Wasted Energy ambao staa wa Marekani, Alicia Keys amemshirikisha, Diamond Platnumz, umesikilizwa na watu wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube kuliko ngoma nyingine zinazopatikana kwenye albamu yake, ALICIA. 

Mapema jana, Alicia Keys aliachia nyimbo 15 kwenye chaneli yake ya YouTube ila jambo la ajabu wimbo, Wasted Energy ambao Diamond ameimba mwishoni kwa sekunde chache ulitazamwa na watu zaidi ya 111,000 ndani ya saa tisa pekee huku kwa Tanzania ukiingia kwenye ‘trending’. 

Wakati wimbo, Wasted Energy ukifikisha idadi hiyo kubwa ya wasikilizaji kwenye YouTube, ngoma zingine zilikuwa zinajikongoja kwa kusikilizwa na watu wachache ambapo wimbo uliosikilizwa zaidi ni 3 Hour Drive wenye ‘views’ 19,000 pekee. 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,649FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles