28.2 C
Dar es Salaam
Monday, July 4, 2022

Diamond afanya kufuru Maulid ya dada yake

 IKIWA leo ndio tukio lenyewe la harusi ya dada wa Diamond Platnumz, Esma Platnumz na mfanyabiashara Msizwa, unaambiwa usiku wa kuamkia jana, msanii huyo alifanya kufuru ya kumwaga mkwanja wa maana alipokuwa anawatuza maharusi.

Diamond aliongoza ndugu zake katika kuwatuza noti maharusi, Esma na mumewe kwenye shughuli Maulid iliyofanyika nyumbani kwake, Madale, Dar es Salaam huku harusi yenyewe ikitarajiwa kufanyika leo, Lugalo Golf Club.

Kabla hajaanza kumwaga fedha, Diamond alisema:“Kwanza nina furaha sana leo ya kumuoza dada yangu lakini furaha ya pili, kutokana na harusi ya dada yangu na mimi itanipa mtu wa kunipenda na mimi nioe, hakuna kitu kinaboa kama kumuozesha dada yako kwa shemeji ambaye hana hela, unapokuwa na dada mzuri kama Esma lazima dada ajiweze, natuza elfu 10 10.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,637FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles