27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Deschamps ashangaa Koscielny kustaafu

PARIS, UFARANSA


KOCHA wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, ameshtushwa na  uamuzi wa kustaafu kucheza michezo ya kimataifa uliotolewa na beki wake, Laurent Koscielny.

Koscielny, ambaye ni beki katika timu ya Arsenal, inayocheza Ligi Kuu England, alitoa uamuzi huo hivi karibuni, wakati akiendelea kuuguza jeraha lake la misuli ya paja ambalo pia lilimfanya kukosa michezo ya Kombe la Dunia.

Hata hivyo, beki huyo alifanya uamuzi huo huku akilalamika kwamba hana mawasiliano mazuri na kocha wa timu ya taifa, Deschamps.

Akizungumzia uamuzi huo wakati wa mkutano na waandishi wa habari juzi, Deschamps alisema: “Ninaelewa hali halisi wakati akizungumzia kuhusu uhusiano, lakini nilishtuka kwa uamuzi wake kama ambavyo wafanyakazi wengine wameshtushwa.”

“Wafanyakazi walionyesha namna ambavyo wameshtushwa. Nilimwita baada ya kupata jeraha, hata alipoamua  kufanyiwa upasuaji nilimwita pia kujumuika nasi wakati wa kujiandaa na michuano ya Kombe la Dunia.

“Septemba mwaka huu ilikuwa siku yake ya kuzaliwa, nilifanikiwa kuzungumza naye kufahamu hali yake kiafya.”

Deschamps  alisema kuwa: “Haitabadilika kuwa Koscielny ni mchezaji  mkubwa ambaye ana thamani duniani.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles