27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dereva wa lori Mtanzania aliyekutwa na corona Uganda kurejeshwa nchini

KAMPALA, UGANDA

DEREVA wa lori mwenye umri wa miaka 34 mkazi wa Dar es salaam ambaye jina lake bado halijatajwa amebainika kuwa na virusi vya corona nchini Uganda.

Tayari mamlaka za nchini humo zimesema zimeanza mchakato kuhakikisha dereva huyo anarejeshwa nchini.

Taarifa zilizochapishwa mtandaoni jana  na gazeti la The Observer  la nchini Uganda zilieleza kuwa kuongezeka kwa Mtanzania huyo kunafanya jumla ya watu walioathirika na virusi vya corona nchini Uganda kufikia 56 kutoka wale 55 waliokuwepo awali.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, dereva huyo wa lori alikuwa ni miongoni mwa watu 1,120 ambao sampuli zao  zilichukuliwa na Taasisi ya Utafiti wa virusi ya Entebbe nchini Uganda. 

Miongoni mwa waliochukuliwa sampuli hizo 744 walikuwa ni madereva wa malori  na wote walibainika hawana maambukizi ya corona isipokuwa dereva huyo ambaye ni Mtanzania.

Pamoja na hao 744 wengine 376 waliochukuliwa sampuli walikuwa ni watu walioko karantini ambao walibainika kukutana na watu wenye corona.

Inaelezwa kuwa dereva huyo Mtanzania aliingia nchini Uganda akipitia katika mpaka wa Mutukula Aprili 16 na serikali ya Uganda imesema utaratibu umekwishaanza kufanyika kumrejesha Tanzania.

Awali kabla ya kukanushwa na Waziri wa Afya wa Uganda, kulikuwa na taarifa kuwa Mtanzania huyo alikuwa anatoka katika jamii ya watu wa Uganda.

Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Afya katika Wizara ya Afya ya Uganda Dk. Henry Mwebesa alikaririwa akisema kuwa timu za uchunguzi zikisaidiwa na vikosi vya usalama zinamtafuta dereva huyo wa lori Mtanzania ili arejeshwe nchini kwa ajili ya matibabu.

Dk. Mwebesa aliongeza kuwa dereva huyo Mtanzania hakuonyesha dalili zozote za kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Huyo  ni dereva wa pili kubainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona nchini Uganda.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limebaini kuwa kesi za waliothibitika kuambukizwa virusi vya corona barani Afrika imegonga kwa kasi na kufikia asilimia 51 katika kipindi cha wiki moja.

WHO imetoa onyo ikisema 

Afrika inaweza kuwa kitovu kinachofuata cha mlipuko wa virusi hivyo.

WHO imetoa onyo hilo  kutokana na kile ilichosema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la visa vya watu wanaokufa na kuambukizwa virusi hivyo katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Kumekuwa na vifo vya karibu watu 1,000 na zaidi ya maambukizi 18,000 katika Bara zima la Afrika hadi sasa, ingawa viwango hivi ni vya chini sana  ukilinganisha na vile vya vinavyotokea katika Bara la Ulaya na Amerika.

Nchini Tanzania idadi ya watu waliobainika kuwa na virusi vya corona imepanda na kufikia 147 baada ya kesi nyigine mpya 53 kutangazwa Ijumaa. 

Nchini Kenya kesi zimepanda na kufikia 246 baada ya sampuli 12 kati ya 450 kuonyesha maambukizi.

Rwanda kesi zimepanda na kufikia 143 baada ya nyingine tano mpya kuongezeka Ijumaa.

Aidha kesi za waliopona zimeongezeka na 

Kuna kesi karibu milioni 2.2 za watu waliothibitika kuambukizwa virusi vya corona duniani na vifo takribani 148,000 .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles