27.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

DEREVA WA BOBI WHINE ADAIWA KUUAWA NA POLISI

Kampala, Uganda

Dereva wa Mbunge Kyadondo Mashariki, Robert Ssentamu maarufu Bobi Whine ameripotiwa kufariki dunia baada ya kupigwa risasi katika mji wa Arua nchini Uganda.

Dereva huyo anaejulikana kama Kawooya Yasin, alipigwa risasi na kuuawa Jumatatu jioni akiwa katika gari eneo la Hoteli ya Pacific baada ya kutokea vurugu katika kampeni za uchaguzi mdogo katika Manispaa ya Mji wa Arua.

Akithibitisha tukio hilo Bobi ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa dereva wake ameuawa na polisi wakidhani ni yeye.

“Askari wamempiga risasi dereva wangu wakidhani ni mimi, hoteli nilipo imezingirwa na askari na wanajeshi wa SFC,” ameandika Bobi Whine.

Bobi Whine yuko katika Mji wa Arua kwa ajili ya kufanya kampeni za mwisho katika kumuunga mkono mgombea ubunge wa ene hilo, Kassiano Wadri.

Polisi hawajathibitisha kuhusika na tukio hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles