25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, October 23, 2021

Dereva atuhumiwa kumuua Konda wakigombea abiria

Na Ramdhan Hassan, Dodoma

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Dereva wa Daladala (jina linahifadhiwa) kwa kosa la mauaji ya Kondakta wa daladala, Juma Hamisi (25) wakati wakigombea abiria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Alhamisi Julai Mosi, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga amesema Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Juni 15, 2021 katika Mtaa wa Mji Mpya jijini Dodoma ambapo alimuua kwa kumpiga na jiwe kichwani wakati wakigombea abiria katika eneo hilo.

Kamanda Lyanga amesema dereva huyo mara baada ya kumuona abiria walianza kumgombea na marehemu kila mmoja akitaka aingie katika gari yake.

Amesema mara baada ya msako Juni 19, mwaka huu wamefanikiwa kumkamata dereva huyo akiwa mafichoni katika Kijiji cha Galapo Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara. Kamanda Lyanga amesema mtuhumiwa anatarajia kufikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji.

Wakati huo huo, Kamanda Lyanga amesema kipaumbele chake ni kulinda raia na mali zao pamoja na kusimamia haki na wajibu huku akiomba ushirikiano kutoka kwa wananchi na raia wema kwa kudai kwamba ofisi yake ipo wazi muda wowote kwa mwenye malalamiko anakaribishwa.

Hatua hiyo inakuja kufuatia hivi karibuni Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP) Simon Sirro kufanya mabadiliko ya Makamanda wa polisi wa mikoa ambapo mkoa wa Dodoma alimchagua Kamanda Lyanga ambaye awali alikuwa Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Rufiji.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,953FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles