31.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

DENNIS RODMAN AREJEA KOREA KASKAZINI

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un na Dennis Rodman wa Marekani wakiangalia mchezo wa mpira wa kikapu mwaka 2013.

 

 

Pyongyang, Korea Kaskazini

ALIYEKUWA nyota wa mpira wa kikapu  Marekani, Dennis Rodman amefanya tena ziara nchini Korea Kaskazini ambayo ina mgogoro mkubwa na Marekani.

Nyota huyo wa zamani wa NBA anafanya ziara ya binafsi kwa mara ya tatu.

“Ninajaribu tu kufungua mlango, nina furaha kuwa Rais Trump anafurahia kwa sababu  mimi niko hapa na ninajaribu kutimiza kitu fulani ambacho sisi sote tunahitaji,” alisema Rodman.

Alikuwa akizungumza na  waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Beijing akielekea   Korea Kaskazini.

Vyombo vya  habari vimeripoti kuwa  Rodman anafanya ziara ya urafiki na kiongozi wa  Korea Kaskazini, Kim Jong-un.  Awali alitembelea nchi hiyo mwaka 2013 na 2014.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema   inafahamu ziara yake.

“Tunamtakia mema  lakini tumetoa onyo kwa raia wa Marekani na kuwashauri wasisafiri kuenda nchini humo kwa usalama wao,” alisema Naibu Waziri wa Mambo ya Mje wa Marekani, Thomas Shannon.

Mgogoro kati ya Marekani na Korea Kaskazini umekuwa mkubwa wakati huu wa utawala wa  Rais Donald Trump, ambaye anasema   anahofia mzozo mkubwa huenda ukaibuka kati ya nchi hizo mbili.

Rais Trump pia amesema kuwa angependa kukutana na Rais Kim wa Korea Kaskazini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles