29.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 17, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

DENI LA DUNIA LAONGEZEKA

Ripoti iliyotolewa na shirika la makundi ya kiraia na kanisa Ujerumani la Jubilee Germany inayozungumzia hali ya madeni kwa mwaka wa 2019 imesema viwango vidogo vya riba na mikopo nafuu vinachochea mataifa masikini zaidi kukopa katika kiwango kisichomithilika na kujikuta yakikabiliwa na madeni makubwa ambayo hushindwa kuyalipa.

Jubilee imeyaangazia mataifa 152 kwenye ripoti hiyo, ambapo 122 miongoni mwake yanakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni mara tatu zaidi ya mwaka 2017.

Ripoti hiyo imesema takriban mataifa yote ya Afrika yameelemewa na madeni, miongoni mwao ni Angola, Gambia, Sao Thome, Somalia, Sudan Kusini na Sudan ambayo yanakabiliwa na hali mbaya zaidi kiasi cha kushindwa kumudu kulipa.

Kufuatia hali hiyo, shirika hilo limetoa mwito wa kuongezwa kwa muda wa kulipwa kwa madeni hayo ama kutolewa kwa nafuu ya madeni kwa mataifa yanayokabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
595,000SubscribersSubscribe

Latest Articles