29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

DEMOCRAT WATAKA MWENDESHA MASHITAKA MAALUM KUMCHUNGUZA TRUMP

WASHINGTON, MAREKANI

IKULU ya Marekani imepuuzilia mbali wito wa Chama cha upinzani cha Democrat wa kutaka kuteuliwa mwendesha mashitaka maalum wa kuchunguza madai kuwa kampeni ya Donald Trump ilishirikiana na Urusi.

Wito huo ulikuja kufuatia hatua ya Rais Trump kumtimua ghafla Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), James Comey kwa madai ya kushindwa kushughulikia sakata la barua pepe za Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Hillary Clinton.

Hatua ya kushtusha ya Trump kumfuta kazi Comey aliyekuwa akisimamia uchunguzi wa madai kuwa Urusi iliingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani 2016 umezusha moto wa kisiasa mjini hapa na kuutumbukiza utawala wake katika mkanganyiko.

Wabunge wa Democratic waliojawa na hasira wanaonya kwamba kazi ya FBI kwa sasa itachafuliwa kabisa na kuvurugwa na siasa, hivyo umuhimu wa kuteuliwa mwendesha mashitaka maalum kuchunguza suala hilo.

Ikulu ya White House ilisema Comey alifutwa kazi kutokana na wasiwasi wa na namna alivyoshughulikia uchunguzi wa barua pepe za Clinton, ambaye alishindwa na Trump katika uchaguzi wa urais mwaka jana.

Trump aliutetea uamuzi wake huku akipinga madai kuwa ulihusishwa na uchunguzi dhidi ya Urusi, akidai Comey hakuwa akifanya kazi vizuri.

Lakini Comey, amejibu hatua hiyo kwa kuwaandikia barua maafisa katika idara hiyo na rafiki zake.

Alisema hatapoteza muda wake juu ya hatua iliyochukuliwa au jinsi ilivyotekelezwa na kuwa kwa muda mrefu aliamini Rais atakuwa na kila sababu ya kumtimua kazini mkurugenzi wa FBI kwa sababa  moja au bila sababu yo yote.

Wakati huo huo, maseneta wanaochunguza uhusiano uliopo kati ya Rais Donald Trump na Urusi wamemwagiza aliyekuwa mshauri wa masuala ya usalama Michael Flynn afike mbele yao kuhojiwa.

Msaidizi huyo wa zamani wa Trump, alilazimishwa kujiuzulu Februari baada ya kusema uongo juu ya mawasiliano yake ya simu na balozi wa Urusi nchini humo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles