25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

DED Iramba ampongeza Dk. Samia kwa kutoa msaada kwa wanufaika wa TASAF

Na Seif Takaza, Iramba

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Michael Matomora amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia Ubalozi wa China kupitia Taasisi ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima kwa kushirikiana na TASAF kuleta vifaa mbalimbali kwa ajili ya Walengwa wa Mpango wa TASAF.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hamashauri ya Wilaya ya Iramba, Michael Matomora akizungumza na walengwa wa Tasaf katika viwanja vya Shule ya Sekondari Shelui.

Matomora ametoa pongezi hizo juzi wakati akiongea na Walengwa wa Mpango wa TASAF waliofika ili kupokea vifaa mbalimbali vilivyotolewa na serikali kupitia Taasisi hizo katika uwanja wa shule ya sekondari Shelui wilayani hapa.

“Nitoe shukrani na pongezi kubwa sana kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia Ubalozi wa China kupitia Taasisi ya Dk. Dorothy Gwajima kwa kushirikiana na TASAF kuleta vifaa vyenye thamani ya Tsh 43.8 milioni,” amesema Matomora.

Aidha, amewataka Walengwa wa Mpango wa TASAF kuvitumia vifaa hivyo kwa ajili ya kuondokana na umasikini huku akiwaasa kutoviuza vifaa hivyo.

“Niwaombe ndugu zangu Walengwa kushirikiana na serikali ili kuondoa umasikini, hivyo pokeeni vifaa hivi na mvitunze ili viwe kumbukumbu katika maisha yenu na kuwa mchango mkubwa katika kuondoa umasikini,” amesema.

Amesema vifaa hivyo vitarahisisha sana uendeshaji wa maisha ya kila siku hatimaye kufikia lengo la Serikali.

“Sitarajii kusikia vifaa hivi vinauzwa ili kukidhi njaa kwa sababu njaa ni rafiki yetu wa maisha, hatutaachana nayo mpaka tunaingia kaburini,” amesema.

Ameongeza kuwa: “Ikitokea mkauza vifaa hivi ili kutatua swala la njaa, je baada ya kuuza vifaa hivyo kesho mtauza nini tena, hivyo mkatumie vifaa hivyo ili kupata manufaa mbalimbali yaliokusudiwa na serikali,” amesema.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amewataka wazazi na walezi kuanza maandalizi ya kuandaa chakula kwa ajili ya wanafunzi ili ifikapo mwakani kuhakikisha wanafunzi katika shule zote wanapata chakula.

“Tutahakikisha kwamba tunawapa watoto hawa chakula kwa sababu watoto hutumia akili ili kupata maarifa, hivyo ili watoto hawa waitumie akili vizuri wanatakiwa wawe wameshiba,” amesema.

Aidha, amewataka wazazi hao kufahamu kuwa elimu bila chakula tumboni mwa mtoto ni sawa na sumu kwa sababu ubongo usiokuwa na chakula hutumika hatimaye kutengeneza watoto wasikuwa na uelewa mpaka ukubwani mwao.

Awali, akiongea katika hafla hiyo fupi mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Zabina Kabaju aliwataka Walengwa hao kuvitumia vifaa hivyo kwa uadilifu na mapenzi makubwa.

“Tunawaomba ndugu zetu walengwa kuzingatia matumizi halali na halisi ya vifaa hivi ili viwasaidie kujiinua kiuchumi,” amesema.

Nae, Aline Augustin ambaye alimwakilisha Dk. Gwajima, aliwataka Walengwa hao kufahamu kuwa Taasisi yao imelenga kuwapunguzia mzingo wa kuandaa vifaa vya wanafunzi hasa katika kipindi hichi ambapo Shule zinafungwa na kufunguliwa Januari.

“Ni hakika Januari wazazi huitajia vifaa mbalimbali vya wanafunzi, hivyo aliwataka kuvitunza vifaa hivyo ili viwasaidie watakapofungua shule mapema mwakani,” amesema.

Upande wao walengwa wa mpango huo wameishukuru Serikali kwa kuwapatia vifaa hivyo huku wakiamini kuwa vitakuwa chachu ya wao kutimiza malengo yao.
wao kupata elimu ambayo itawafanya wafikie malengo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles