DED awataka vijana kuchangamkia viwanja

0
1225

godwin-kunambiNa RAMADHAN HASSAN

-DODOMA

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi, amewataka vijana wa mkoa huo kutumia fursa ya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kwa kutafuta ardhi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kunambi alisema vijana wa Mkoa wa Dodoma wanatakiwa kuchangamkia fursa ya kununua ardhi kwa ajili ya kuwekeza kutokana na mkoa huo kuwa makao makuu.

Alisema wanatakiwa kuacha utaratibu wa kulalamika kuwa fursa zinawapita mbali na badala yake wanatakiwa kuitumia nafasi hiyo ili kujijenga kiuchumi.

“Mimi ni mgeni katika mkoa huu ila na mimi ni kijana hivyo nawaomba vijana wenzangu kujikita katika kununua ardhi kwani kuna watu najua watakuja kutaka kununua hivyo kijana ni lazima awe wa kwanza katika kila kitu,” alisema.

DED huyo ambaye aliteuliwa hivi karibuni na Rais Dk. John Magufuli, alitoa wito kwa vijana kuwa waangalifu katika mahusiano yao kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa Ukimwi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here