23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Deco awataka Man United kumsikiliza Mourinho

decoMANCHESTER, ENGLAND

NYOTA wa zamani wa klabu ya Barcelona, Anderson de Souza (Deco), amewataka wachezaji wa klabu ya Manchester United kumsikiliza kwa makini kocha wao, Jose Mourinho kwa ajili ya kupigania ushindi katika michezo yao ijayo.

Deco amewahi kuwa chini ya kocha huyo mwaka 2004 katika klabu ya Porto ya nchini Ureno, hivyo Deco anaamini kuwa wachezaji wa Manchester United wanashindwa kufanya vizuri kutokana na kutomsikiliza kwa makini kocha huyo.

Inadaiwa kwamba, Mourinho amekuwa mkali sana kwa wachezaji wake, hivyo kuna baadhi ya wachezaji wanadai kuwa wananyanyaswa na ndio maana wanashindwa kufanya vizuri.

“Kama unapata nafasi ya kuja kucheza katika klabu kubwa kama vile Chelsea, Manchester United, Barcelona na Real Madrid unatakiwa kujiandaa mwenyewe kuwa katika kiwango bora na unatakiwa kukubaliana na kila hali.

“Hata mimi kwa upande wangu sipendi kocha akiwa mkali na mbaguzi, lakini najua kwamba siku zote anajua kuliko sasa na ninaamini kuwa kuna wakati kocha anafanya hivyo si kwa ajili ya kuwanyanyasa lakini ni kwa ajili ya kuwabadilisha.

“Anachokifanya kwa sasa Mourinho ni kuhakikisha timu yake inafanya vizuri katika michezo yake na kupigania mataji, hivyo wachezaji wanatakiwa kumuunga mkono kocha wao na kumsikiliza kwa makini kwa ajili ya kuhakikisha wanatimiza malengo ya timu,” alisema Deco.

Hata hivyo, Deco amedai kuwa hata wakati kocha huyo anaifundisha klabu ya Porto, alikuwa na tabia hiyo ya kuwasema wachezaji na walikuwa wanachukia, lakini mwisho wa siku walikuwa wanapambana kwa ajili ya timu na wakawa wanafanikiwa kushinda.

“Kocha hata kama akiwasema wachezaji kupitia vyombo vya habari au chumba cha kubadilishia nguo juu ya timu kushindwa kufanya vizuri yote ni yale yale wachezaji wanaguswa,” aliongeza Deco.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles