DECI MPYA YAIBUKA NCHINI

0
1041
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango

 

 

MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

WAKATI baadhi ya taasisi na nchi jirani zikiwaonya wananchi wake dhidi ya upatu uitwao D9 Club unaofanana na Deci, uliopigwa marufuku miaka kadhaa iliyopita, Serikali imeshindwa kutoa kauli kama unaruhusiwa nchini au hauruhusiwi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alipoulizwa endapo Serikali ina taarifa za mchezo huo, alisema kwa sasa hawezi kuzungumza chochote hadi baada ya bajeti kuu ya Serikali kupitishwa na Bunge.

Tangu kuingia kwa upatu huo ambao asili yake ni Brazil na ambao unafanya kazi kwa kutumia mfumo wa bitcoin, watu wananunua na kuuza hisa kwa njia ya mtandao.

Kutokana na hali hiyo, watu mbalimbali wamekuwa wakiweka mamilioni ya fedha kwa matumaini ya kupata zaidi ndani ya muda mfupi.

D9 au D9 SPORT Trading kama unavyojulikana na wengi, ni biashara ya kuuza na kununua hisa za michezo ya kimataifa ambayo mwanachama anapata faida kila wiki kulingana na hisa zake kwenye kampuni.

Kupitia mchezo huo, kampuni hupata faida kutokana na wataalamu wa kubahatisha matokeo ya michezo ya kimataifa ambapo anayenunua hisa, hupata faida hiyo bila kubahatisha moja kwa moja michezo hiyo.

Ndani ya D9 Club kuna njia mbili za kufanya kazi na kupata faida, moja ni kuwekeza hisa na kupata faida kwa kila wiki na ya pili ni kufungua akaunti kwa Dola 50 za Marekani na kufundisha wengine ili wajiunge na kila anayejiunga unapewa pointi.

Kwa wanaonunua hisa, wapo kwenye makundi manne, kundi la kwanza ni bronze lenye Dola 302, kundi la pili ni Silver lenye Dola 561, kundi la tatu ni Gold ambalo kujiunga ni Dola 1,070 na la mwisho ni Gold+  ambalo kujiunga ni Dola 2,086.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here