26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

DC Sabaya azitaka benki kuiga NMB kusaidia wajawazito Hai

Omary Mlekwa, Hai

Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro , Lengai Ole Sabaya amezitaka benki na taasisi mbalimbali nchini kuiga mfano wa Benki ya NMB katika kutoa misaada kwa jamii.

Sabaya amesema hayo katika Kata ya Machame Magharibi, wakati akipokea vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani y ash milioni 10 vikiwamo vitanda 12 vya kujifungulia vilivyotolewa na benki hiyo, Ole Sabaya  amesema kuwa awali hospitali hiyo ilikuwa na changamoto ya vitanda kwa ajili ya kinamama kujifungulia lakini kutokana na msaada huo tatizo hilo limebaki kuwa historia .

“Naipongeza benki ya NMB kwa kutambua thamani ya kinamama wa  Hai ingawa katika nchi yetu kuna changamoto nyingi sehemu zingine lakini ninyi mmeamua kutuletea misaada huu katika halmashauli yetu.

“Mimi nawatia moyo tu kwa niaba ya wananchi wa Hai msichoke kutusaidia kwani mahitaji yetu bado ni mengi ingawa nasi kama serikali tunapambana ili kuihakikisha kinamama wanajifungua bila matatizo ya aina yeyote hile ndio maana hata vifo vya kinamama kata ya Machame Magharibi  wakiwa wanajifungua vinazidi kubaki kuwa historia,” amesema Sabaya.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Dk. Irene Haule  amesema vifaa hivyo vimekuja kwa muda mwafaka kutokana na maombi yao. 

 “Napenda kuwaomba watumishi wa idara ya afya katika halmashauri yetu  kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anapambana ili kuwasaidia wagonjwa wanaokuja kupata huduma  kuongoza kwa utoaji wa huduma za kiafya hapa nchini,” amesema Dk. Haule.

Naye Meneja wa Benk ya NMB Kanda ya kaskazini,  Aikansia Muro amesema benki hiyo imetoa msaada huo kwa lengo la kutoa faida wanazozipata kwa jamii ili kuisaidia serikali baadhi ya changamoto zinazokuwa zikiwakabili wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles