29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

DC Rombo akamata fuso lenye simu za magendo

Na MWANDISHI WETU -ROMBO

MKUU wa Wilaya ya Rombo, Dk. Athumani Kihamia akiambatana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo, Meneja msaidizi na watumishi wa Mam- laka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, mwishoni mwa wiki wamekamata fuso lililokuwa lime- beba maboksi ya simu yenye tham- ani ya zaidi ya shilingi milioni 700.

Kwa mujibu wa Dk. Kihamia, simu hizo ambazo zilikuwa zimepa- kiwa kwenye fuso lenye namba za usajili T 386 BQZ ambazo zilikuwa zimefunikwa na mikungu ya ndizi zilikua na lengo la kupitishwa kima- gendo kupelekwa Dar es salaam jambo ambalo si sahihi kwa mujibu wa sheria za nchi.

Dk.Kihamia alisema kufanya magendo sio vizuri kwa sababu bidhaa hizo zinaweza kuwa hazina ubora kwa watumiaji na walaji, pia zinapoteza mapato kwa taifa kwa kuwa zinakwepeshwa kulipiwa kodi

na kulifanya taifa kupoteza mapato yake.Aliongeza kuwa hayo mapato ambayo wafanyabiashara wanak- wepa yanakosesha kodi ambazo zingeweza kusaidia jamii katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na huduma nyingine za jamii katika wilaya hiyo na taifa kwa ujumla.

“Kwa kupitisha mizigo kima- gendo kama hivi kukwepa na kodi ni sawa na uhujumu uchumi na ni kosa kubwa na adhabu yake ni pamoja na kutaifishwa au faini ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ovu ya kufanya kitu kama hicho, “ alisema Kihamia.

Kihamia alisema Wilaya ya Rombo ipo mpakani mwa nchi ji- rani ya Kenya na watu wamekuwa wakitumia kupitisha vitu visivyo- halali hivyo aliwaasa kuacha hivyo Mara moja.

“Si mizigo tu hapo Tarakea pal- ipokamatwa mizigo hata maeneo mengine ikiwemo Holili pakuwa na matukio hayo na si mizigo tu hata biashara ya wahamiaji haramu, tu- naendelea na operesheni hizi mara

kwa mara kuwabaini na kuwadhibiti wahusika wote,” alisema Kihamia.

Akizungumzia waliohusika na tukio hilo alisema tayari dereva wa fuso (jina limehifadhuwa) name- kamatwa pamoja na wahusika wen- gine ambao ni wanawake.

Aliongeza kuwa baadhi ya wa- nawake wamekuwa wakitumika ka- tika kufanya vitendo hivyo kwa ku- jifanya wanasafirisha ndizi kumbe wamepakia na mizigo mingine ya magendo.

Aliongeza kuwa anawaasa akina mama kuacha tabia hizo zitakuja kuwaweka pabaya , na kuasa asije kusikia wakilalamika wakati waki- fanyiwa ukaguzi kwa kuwa wame- kuwa wakijihusisha na vitendo hivyo.

“Serikali iko macho kuliko mna- vyofikiria msijaribu fanyeni biasha- ra zenu kihalali ili serikali inufaike na mfanyabiashara anufaike pia, “

“Serikali inawashukuru wa- nanchi kwa ushirikiano walioone- sha katika kufichua maovu hayo yal- iyokuwa yakifanywa na nawaahidi muendelee kuwafichua kila mkihisi

hakunà uhalali kwenye biashara zinapopitishwa mipakani mwetu, na kwamba wote wanaowafichua wahalifu watakuwa katika mikono salama kwa kutunziwa siri” al- iongeza Kihamia.

Ikumbukwe mnamo tarehe 20 julai 2020 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua Rais Dkt. John Pombe Magufuli al- imwagiza mkuu huyo wa wilaya ya Rombo kwenda kusimamia haki za wanaodhulumiwa na kuzuia magendo katika wilaya ya Rombo, ambapo utekelezaji wake umeanza kuonekana.

Naye Meneja TRA, Gabriel Mwayozi alisema njia za magendo si sahihi kutumia kwa mfanyabiashara kwa kuwa zinaharibu soko la walipa kodi lakini pia kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kukusanya kodi za mapato.

Meneja huyo ameahidi kush- irikiana na uongozi wa wilaya ya Rombo kukomesha kabisa magen- do yote mipakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles