29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

DC Pangani kuwapa wazee 1,700 vitambulisho vya matibabu

Mwandishi Wetu, Pangani     



Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah, atakabidhi vitambuzisho zaidi ya 1,700 kwa wazee wilayani humo.

Lengo la kutoa vitambulisho hivyo ni kuwashukuru wazee hao kwa kazi nzito waliyofanya hadi sasa katika kuijenga Pangani na taifa kwa ujumla kuelekea siku ya wazee duniani ambayo hufanyika Oktoba Mosi kila mwaka.

Amesema hatua hiyo kwa wazee ni zawadi ya uhakika katika sekta ya afya kama jambo muhimu zaidi kwao hasa nyakati hizi ikiwa ni kuhakikisha wazee wote ndani ya siku tatu wanapata vitambulisho vyao vya matibabu bure kama ilivyoelekezwa na serikali ya awamu ya tano.

“Hizi ni shukrani zetu kwa wazee ambapo pamoja na mambo mengine ndani ya siku tatu kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba Mosi ambayo ni siku ya kilele, watapatiwa bure matibabu kama vile upasuaji vipimo na matibabu bure maalumu toka kwa wataalamu ndani na nje ya Pangani.

“Kwa watakaopatikana na matatizo ya macho watapatiwa miwani, dhamira yetu ni kuwajengea uwezo na kuwapa tumaini jipya na mikakati ya serikali juu yao ikiwamo kujua kero na changamoto zao kutafutiwa ufumbuzi,” amesema Zainab.

Pamoja na mambo mengine, Mkuu huyo wa wilaya amesema katika siku ya kilele atapata chakula cha mchana na wazee hao nyumbani kwake pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles