23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

DC Moshi ahamasisha wananchi kujiandikisha daftari la wapiga kura

Upendo Mosha, Moshi

Mkuu wa wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Kippi Warioba ameendelea  kupita katika maeneo mbalimbali ikiwemo viwandani pamoja na vyuoni na kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.

Mkuu huyo wa wilaya ambaye aliongozana na kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo, leo Oktoba 16, ailipita na kufanya ukaguzi wa vituo vya kupigia kura katika kiwanda cha sukari cha TPC pamoja na Chuo kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).

Akizungumza wakati akihamashisha wananchi hao kujiandikisha katika daftari hilo na kujitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba amesema ni jukumu na wajibu wa kila mwananchi kushiriki katika uchaguzi huo.

“Kila mwananchi anapaswa kujiandikisha katika daftari hili lengo ni yeye kuhakikisha anashiriki katika uchaguzi na kuwachagua viongozi wa vijiji na vitongojo jambo ambalo ni muhumu katika maendeleo yetu Kama wilaya na taifa kwa ujumla.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya ameonyeshwa kufurahishwa na Kasi ya uandikishaji katika vituo hivyo ambapo aliwagiza wakuu wa idara katika halimshauri ya Moshi kuhakikisha watumishi wote wamejiandikisha katika daftari hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles