26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Dc Maswa aridhishwa na kasi ya RUWASA

Na Samwel Mwanga, Maswa

MKUU wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Aswege Kaminyoge ameonyesha kuridhishwa na ujenzi wa Miradi ya maji inayotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira(RUWASA)wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Aswege Kaminyoge(mwenye kaunda suti)akizungumza na wananchi aliowakuta wakichota maji kwenye kituo cha kuchotea maji kwenye zahanati ya kijiji cha Isanga wakati akikagua mradi wa maji wa Isanga unaotekelezwa na Ruwasa.(Picha Na Samwel Mwanga).

Kaminyoge amesema hayo mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya maji ya Vijiji vya  Inenwa-Kizungu na ule wa kijiji cha Isanga ambapo aliongozana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo.

Amesema kuwa serikali imetoa fedha nyingi wilayani humo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji hasa ya maeneo ya vijijini ili kumshusha mama ndoo  kichwani.

Amesema kwa sasa ujenzi wa miradi hiyo imefikia hatua nzuri na kuwataka kuongeza kasi ya Usimamizi wa miradi hiyo kwa kazi ndogondogo zilizobakia ili wananchi wanufaike nayo kwa kupata maji safi na salama.

“Miradi hii yote ya maji ambayo Ruwasa mnaisimamia na sisi wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya tumeitembelea kwa kweli tumeridhika na maendeleo ya ujenzi wake ila sasa kwa zile kazi ndogondogo zilizobaki hakikisheni mnasimamia zinamalizika haraka ili wananchi wanufaike kwa kupata maji safi na salama.

“Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu imetoa fedha nyingi katika kutekeleza miradi ya maji katika wilaya yetu kwa mradi wa Inenwa–Kizungu Sh nilioni 469 zimetolewa na mradi wa Isanga Sh Milioni 534 zimeletwa na serikali hivyo tunachotaka kuona ni wananchi wanapata maji safi na salama,” amesema Kaminyonge.

Aidha, amesema na miradi mingine ya maji iliyoko kwenye wilaya hiyo inayotekelezwa na Ruwasa ni vizuri kasi ya usimamizi ikaongezwa ili iweze kukamilika kwa wakati na kupunguza adha ya wakinamama kufuata maji umbali mrefu. 

Meneja wa Ruwasa wilaya ya Maswa, Mhandisi Lucas Madaha amesema licha ya changamoto chache zilizopo wameweza kukabiliana nazo kwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa shughuli zilizobaki ili miradi hiyo yote ikamilike kwa muda ambao wamepangiwa.

Amesema kwa sasa ujenzi wa miradi hiyo imefikia hatua nzuri na kuwataka kuongeza kasi ya Usimamizi wa Miradi hiyo kwa kazi ndogondogo zilizobakia ili wananchi wanufaike nayo kwa kupata maji safi na salama.

“Miradi hii yote ya maji ambayo Ruwasa mnaisimamia na sisi wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya tumeitembelea kwa kweli tumeridhika na maendeleo ya ujenzi wake ila sasa kwa zile kazi ndogondogo zilizobaki hakikisheni mnasimamia zinamalizika haraka ili wananchi wanufaike kwa kupata maji safi na salama.

 “Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu imetoa fedha nyingi katika kutekeleza miradi ya maji katika wilaya yetu kwa mradi wa Inenwa-Kizungu Sh milioni 469 zimetolewa na mradi wa Isanga Sh milioni 534 zimeletwa na serikali hivyo tunachotaka kuona ni wananchi wanapata maji safi na salama,”amesema Mhandisi Madaha.

Aidha, ameongeza kuwa miradi mingine ya maji iliyoko kwenye wilaya hiyo inayotekelezwa na Ruwasa ni vizuri kasi ya usimamizi ikaongezwa ili iweze kukamilika kwa wakati na kupunguza adha ya wakinamama kufuata maji umbali mrefu. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles