24.6 C
Dar es Salaam
Thursday, December 2, 2021

DC Kiteto anusuru mgogoro wa shamba kati ya serikali ya kijiji, uongozi CCM

Mohamed Hamad, Kiteto

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhandisi Tumaini Magesa, amenusuru mapigano yaliyotaka kutokea kati ya wanachama wa CCM Kata ya Kijungu na Serikali ya Kijiji kugombea shamba la ekari 155.

Akizungunza na pande zote mbili katika kikao maalumu kijijini hapo, Mhandisi Magesa jana alizitaka pande hizo kutofanya shughuli yoyote katika shamba hilo ndani ya siku 10 hadi atakapotoa maelekezo.

“Serikali inatamani kuona wananchi mkiishi kwa amani, mkifanya shughuli bila bughudha, sasa hapa naona kunaashiria uvunjifu wa amani.

“Naagiza mtu yeyote asikanyage pale shambani hadi mtakapopata maelekezo mengine,” amesema DC Magesa.

Amesema makundi hayo yanatishiana kuchomeana trekta itakayofika kulima shambani hapo na kuongeza kuwa kamwe hatamani kuona vurugu hizo zikitokea.

Hatu uongozi wa CCM kudai shamba hilo ni la kwao huku Serikali ya Kijiji ikisema ni lao umekuja muda mfupi baada ya uhakiki wa mali za chama hicho na juda ni mali yao.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,646FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles