DC KIGAMBONI: SIJATEULIWA KUONGOZA MAPORI

0
1062

|Nora Damian, Dar es SalaamMkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, amesema hajateuliwa kuongoza mashamba pori ambapo ametishia kuyanyang’anya yale ambayo hayajaendelezwa.

Akizungumza leo wakati wa ziara ya kujitambulisha kwa wananchi na watendaji katika Kata ya Pemba Mnazi, amesema watayarejesha mashamba yote ambayo hayajaendelezwa katika kata hiyo na kupangiwa matumizi mengine.

“Siwezi kuwa mkuu wa wilaya ya mapori, nimetumwa kutatua kero za wananchi. Kama mtu ana eneo lake aje aliendeleze zaidi ya hapo tunanyang’anya,” amesema Sara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here