31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

DC KIGAMBONI: MAPORI YASIYOENDELEZWA KUREJESHWA SERIKALINI

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri

Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM


MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, amesema mapori yote ambayo hayajaendelezwa katika Kata za Pemba Mnazi na Kimbiji yatarejeshwa na kupangiwa matumizi mengine.

Kata ya Pemba Mnazi ina mitaa 15, wakati ya Kimbiji ina mitaa sita na sehemu yake kubwa imegeuka na kuwa mashamba pori kutokana na walionunua kutoyaendeleza.

Akizungumza kwa nyakati tofauti hivi karibuni katika mikutano ya hadhara na wananchi wa kata hizo, alisema hawezi kuwa mkuu wa wilaya ya mapori kwa sababu ametumwa kutatua kero za wananchi.

“Sijaja kuongoza au kulinda pori la mtu, tutayarejesha maeneo yote wenye nia ya kuwekeza wawekeze na ambayo hayatajulikana yatapangiwa matumizi mengine,” alisema Sara.

Aliwaagiza watendaji wa mitaa katika kata hizo waorodheshe mapori ambayo hayajaendelezwa na kwa yale yasiyofahamika waitishe mikutano ya wananchi kuweza kuyabainisha.

“Orodhesheni maeneo yote na muainishe wahusika waliyapata lini, yameendelezwa kwa asilimia ngapi na kama hayajaendelezwa mseme,” alisema.

Awali baadhi ya wenyeviti na watendaji wa mitaa walilalamikia kukithiri kwa wanyama waharibifu wa mazao kutokana na mashamba pori.

Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Kunasenta, uliopo Kata ya Pemba Mnazi, Banyanga Juma, alisema mazao yamekuwa yakiharibiwa na nyani, ngedere, nguruwe pori na vicheche.

Naye Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda katika Kata ya Kimbiji, Ally Kassim, aliiomba Serikali kudhibiti mauaji na wizi wa pikipiki uliokithiri katika maeneo yao.

Naye mkazi wa Mtaa wa Mahenge, uliopo Kata ya Pemba Mnazi, Ashura Haruna, alilalamikia ukosefu wa umeme, licha ya kujitolea kukata mazao yake.

Akijibu kero hiyo, Diwani wa Kata ya Pemba Mnazi, ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Kigamboni, Maabad Hoja (CCM), alisema walifuatilia Tanesco na kuambiwa kuwa mtaa huo na mingine iko katika mchakato wa kuwekewa umeme, lakini changamoto ni upatikanaji wa vifaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles