24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

DC Ileje azionya Halamashauri za vijiji kuwatoza wananchi faini kiholela

Na Denis Sikonde, Songwe

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Anna Gidarya amezionya Halmashauri za vijiji wilayani humo kuacha kupitisha michango bila kuwashirikisha wananchi hali ambayo inaleta mkanganyiko kwa wananchi katika kushiriki baadhi ya shughuli za maendeleo.

Gidarya ameyasema hayo Mei 6, mwaka huu wakati wa ziara yake ya kumsikiliza kero za wananchi katika kijiji cha Mapogoro kata ya Mbebe wilayani humo ambapo hoja za wajumbe wa halmashauri ya kijiji  ni upitishaji wa michango bila kuwashirikisha wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Anna Gidarya akizungumza na wananchi.

Aidha, Gidarya amesema migogoro ndani ya vijiji huibuka kutokana na viongozi wa vijiji na halmashauri zake kupitisha vipaumbele bila kuwashirikisha wananchi kupitia mikutano, ambapo amewataka kuacha kuwatoza faini kwani jambo hilo kimekuwa ni kikwazo kwa wananchi.

Gidarya amesema halmashauri za vijiji, watendaji pamoja na  wenyeviti wa vijiji kwanza wanatakiwa kupitisha  vipaumbele ndani ya vijiji vyao na baadae kupeleka Katika mkutano wa hadhara Ili wananchi wawe wanaelewa na kuacha tabia ya kuwakandamiza na kuwatoza faini zisizo na tija.

Gidarya aliwaonya watendaji na wenyeviti wa vijiji kuacha kugeuza ofisi zao kuwa mahakama, bali wawe washirikishaji wa vipaumbele kwani baadhi yao hufanya kazi za maendeleo bila kuwashirikisha wananchi nini serikali inafanya.

“Vongozi wa vijiji na halmashauri zake washirikisheni wananchi na tengenezeni muundo bora wa utekelezaji ya shughuli za maendeleo na si kuwatoza faini ambazo zinawafanya baadhi ya wananchi kuanza kujificha na  kukwepa maendeleo.

“Wananchi kuchangia fedha za miradi ya maendeleo si kosa, kosa ni kutowashirikisha, hivyo naagiza kiongozi atakaye watoza faini wananchi bila kuwashirikisha nitawashughulikia,” amesema Gidarya.

Mkuu huyo wa wilaya aliwaonya pia wananchi kuacha kutengeneza makundi ya kususia maendeleo, kwani miradi hiyo ni kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vya baadaye, hivyo waendeleei kuunga mkono juhudi za serikali kadri miradi inavyopelekwa kwenye kijiji chao.

Upande wake Diwani wa Kata hiyo, Katofani Mtafya amesema kuanzia sasa ushirikishwaji kwenye  miradi na michango uanzie kwenye halmashauri za vijiji na kuidhinishwa na mikutano ya hadhara Ili kuondoa sintonfahamu ya uendelezaji wa miradi kupitia nguvu za wananchi.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Baraka Mtafya alisema siasa ndani ya kijiji chake zinakwisha utekelezaji wa miradi licha ya wananchi kudai ushirikishwaji haupo, hivyo amewasihi wananchi kuendelea kushirikiana na pindi wanapoiona changamoto wazifikishe ofisini ili kuzitatua.

Goodwin Mlungu ni  mwananchi wa kijiji hicho ambapo alisema viongozi wa vijiji na halmashauri yake hawawashirikishi wananchi mipango ya Kijiji ,hali ambayo huleta sintonfahamu ya kuendeleza miradi ndani ya Kijiji.

“Tunatozwa michango ambayo hatushirikishi ,pamoja na kutosomewa mapato na matumizi kwa kitendo hicho hatutaweza kuendeleza kijiji chetu bila ushirikishwaji,” alisema Mlungu.
PICHA YA KWANZA NA YA PILI NI MKUU WA WILAYA KWENYE MKITANO
PICHA YA TATU SEHEMU YA WANANCHI KWENYE MKUTANO

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles