29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

DC Ileje apiga marufuku wananchi kutozwa faini kiholela

Na Denis Sikonde, Songwe

Faini holela wanazotozwa wananchi kinyume cha sheria kumesababisha Mkuu wa Wilaya Ileje mkoani Songwe, Anna Gidarya kuingilia kati na kumaliza mgogoro huo kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Malangali Kata ya Malangali wilayani humo.

Wakizungumza kwenye mkutano huo Agosti 10, 2022 wananchi hao wameeleza namna faini hizo zinavyotozwa kiholela huku wakihitaji ufafanuzi kutoka kwa mwanasheria wa Halmashauri ili kujua uhalali wa faini hizo.

Antony Kibona ni mkazi wa Kijiji hicho ambapo amesema kuwa kutokufahamu sheria imekuwa mwanya kwa viongozi hao kuwapiga faini bila kujua kosa lao hali ambayo imekuwa kero.

“Kutokujua sheria imekuwa sehemu ya kutupiga faini tukiambiwa tutoe fedha ya mgambo kuanzia Sh 10,000 fedha ya usumbufu (meza) 20,000 sambamba na kuamuliwa kuwekwa ndani,” amesema Kibona. 

Sara Mlungu amesema watendaji wa vijiji wamegeuza ofisi zao kama mahakama ya kutoa hukumu kwa kila mwananchi atakayefikishwa ofsini hapo.

“Tunakuomba mkuu wa wilaya utusaidie wananchi wako ili kuhakikisha wananchi tunaishi Kwa amani na sisi tupo tayari kushirikiana na serikali kwenye shughuli za maendeleo katika maeneo yao,” amesema Mlungu.

Akifafanua juu ya faini zinazotozwa kwenye kata hiyo Mwanasheria wa halmashauri hiyo, Casmir Msofu amesema kila Kijiji na Mitaa ina sheria ndogondogo hivyo zinatakiwa zifuatwe bila kukiukwa.

Msofu amesema faini za kiholela ikiwepo kumlipisha faini mwananchi Sh 10,000 kwa kutohudhuria kwenye maendeleo ni kosa kisheria.

Akitoa kauli ya Serikali Mkuu wa wilaya ya Ileje, Anna Gidarya amewapiga marufuku viongozi kutoa hukumu na kulipisha faini wananchi bila kufuata miongozo.

 “Wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata acheni kutumia nafasi ya ujumbe kuwatoza wananchi faini ambazo hazipo kisheria, mnatakiwa kutoa mapendekezo ya ushauri kwenye mabaraza ya ardhi ya wilaya kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi,”amesema Gidarya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,335FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles