23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

DC Ileje aja na mkakati kudhibiti udumavu

*Ataka kampeni ya lishe kuwa ajenda ya kila kijiji

Na Denis Sinkonde, Songwe

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Anna Gidarya amesema ili kukabiliana na tatizo la udumavu wilayani humo,amemuagiza Afisa Lishe wa wilaya kuandaa fomu maalumu itakayotumika kwa kila Mtendaji wa Kijiji kutuma taarifa za tathimini ya kukabiliana na udumavu kwa watoto chini ya miaka 5.

Sehemu ya wajumbe wa lishe wakiwa kwenye kikao kushuhudia kusaini mkataba.

Gidarya amesema hayo Oktoba 27, 2022 ofisini kwake wakati akitia saini mkataba wa lishe wa kutokomeza udumavu wa kwa watoto chini ya umri wa miaka 5.

Amesema Ileje ni miongoni mwa wilaya ambayo huzalisha mazao ya chakula lakini asilimia 43.3 ya watoto chini ya miaka 5 wana udumavu hali ambayo elimu inapaswa kutolewa na kuwa ajenda kwa kila Kijiji.

“Wananchi wanazalisha vyakula vingi lakini wengi wamejikita zaidi kwenye uchumi badala ya kutumia kwenye chakula na watoto kula vyakula ambavyo vinawasababishia udumavu.

“Nakuagiza Afisa Lishe hakikisha unaanda fomu na kugawa kwa kila mtendaji wa kijiji itakayosaidia kuunda mnyororo wa utoaji taarifa ya namna ya kukabiliana na udumavu na kila mzazi ahakikishe anawapa watoto wake mlo kamili,” amesema Gidarya.

Gidarya amesema wilaya hiyo itahakikisha inatumia majukwaa mbalimbali kuanzia ngazi ya Kijiji, kata, tarafa mpaka wilaya kuandaa makongamano ya kutoa elimu Kwa jamii kukabiliana na udumavu.

Afisa Lishe wilayani humo, Mery Baraka amesema asilimia 43.3 ya watoto waliochini ya miaka 5 wanaishi na udumavu, hivyo serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha elimu inatolewa kwa jamii namna ya kukabiliana na tatizo ikiwepo kuandaa fomu ya ufuatiliaji ngazi ya kijiji pamoja na kila kijiji wataalamu wa afya kutoa elimu.

“Kweli changamoto ya udumavu no kubwa wilayani hapa ambapo kati ya watoto 100 kati yao 43 wana udumavu,” amesema Mery.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ileje, Godfrey Mnauye amesema wapo tayari kukabiliana na tatizo la udumavu, kwa kila fedha inayotolewa na serikali kuelekezwa sehemu husika Ili kuokoa kizazi cha Ileje cha leo, kesho na keshokutwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles